Sambaza....

Inawezekana ikawa ni moja ya bahati ambayo sisi Watanzania tumeanza kuzipata kwa Siku za hivi karibuni kutokana na baadhi ya wachezaji kuwa wanacheza nje ya nchi , tuachane na Samatta Mbwana ambaye ndiye nyota , kuna kuna Msuva Simon , Adi Yusuph ambaye yuko England.

Orodha inazidi kuongezeka kwa sasa hivi baada ya mchezaji mwingine mwenye asili ya Tanzania kusajiliwa na klabu ya Portsmouth ya England. Mchezaji huyo ni Haji Mnoga.

Baba mzazi wa mchezaji huyo ni raia wa Tanzania aliyezaliwa na kuishi Zanzibar , baba mzazi wa Haji Mnoga aliwahi kuwa mchezaji wa mpira wa miguu na alifanikiwa kucheza katika kikosi cha timu ya taifa cha wachezaji waliochini ya umri wa miaka 17 .

Mama yake Haji Mnoga ni wa England na ameishi sana England na Haji Mnoga. Mpaka sasa hivi Haji Mnoga amefanikiwa kucheza mechi moja ya timu ya taifa ya England ya vijana waliochini ya umri wa miaka 17.

Alizaliwa mwaka 2002 , ana miaka 17 mpaka sasa. Kucheza kwake kwenye timu ya taifa ya vijana ya England hakumnyimi yeye kucheza katika timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars.

Bado ana nafasi ya yeye kuchagua timu ya wakubwa ya kucheza  Kati ya England na Tanzania . Shirikisho la soka la Tanzania (TFF) wanatakiwa kuchukua hatua kwa sasa ili kumshawishi achague kuchezea timu ya taifa ya Tanzania.

Haji Mnoga anauwezo wa kucheza kama beki wa Kati pia anauwezo wa kucheza kama beki wa pembeni kulia. Mpaka sasa hivi amefanikiwa kuchukua taji moja la EFL.

Sambaza....