Mchezo wa kufuzu michuano ya Afcon 2023 nchini Ivory Coast kati ya Uganda “The Cranes” na Tanzania “Taifa Stars umemalizika kwa Taifa Stars kuibuka na ushindi wakiwa ugenini.
Ndoto za kufuzu michuano hiyo itakayofanyika mapema mwakani nchini Ivory Coast imeendelea kuwepo baada ya bao safi kutoka kwa Simon Msuva ambae hata hivyo hakuweza kumaliza mchezo huo kutokana na majeraha.
Goli hilo pekee la Stars lilipatikana katika dakika ya 67 kwa Msuva kuunganisha krosi safi kutoka kwa Dickson Job ambae alipokea pasi safi kutoka kwa Mzamiru Yassin baada ya Stars kugongena pasi zakutosha.
Kwa matokeo hayo sasa Taifa Stars wanashika nafasi ya pili wakiwa na alama 4 nyuma ya Algeria wenye alama 9 ambao ndio vinara wa kundi lao ambao hawajafungwa mpaka sasa. Niger wana alama mbili wakiwa nafasi ya tatu wakati Uganda anaburuza mkia na alama moja.
Stars na Uganda sasa watarudiana katika Dimba la Benjamin Mkapa Machi 28 Jumanne saa moja usiku. Ili Tanzania iendelee kuweka hai matumaini yake yakufuzu ni lazima Stars wapate ushindi ili kufikisha alama 7 na kuzidi kuididimiza washinda wakubwa wa nafasi ya pili Uganda.
Kwingineko katika kundi hilo la Stars vinara Algeria wamefanikiwa kuifunga Algeria kwa mabao mawili kwa moja na hivyo kuzidi kujikita kileleni.