Sambaza....

Jadon Malik Sacho kinda wa mwaka 2000 nusu Mtrinidad nusu Mtobago kijana anayechipukia kwa kasi sana kunako medani ya soka akiwa na chama la Borussia Dortmund na timu ya taifa Uingereza.

Nchini Ujerumani ukiulizia Sancho ni nani watakwambia usimuite Sancho sema ‘The Rocket ”, lakini ukisafiri mpaka London kusini ukaulizia hivyo watakwambia sisi huyu dogo tunamuita ‘a ball entertainer’ hii ni kwasababu alikua anawatizama na kuwaiga sana Ronaldinho na Neymar.

Akiwa na umri wa miaka 11, Sancho alikataa ofa ya kujiunga kwenye akademi za Chelsea na Arsenal akuamua kwenda zake Watford alikoamini ni bora zaidi, hapa wazazi wake walimshangaa ila wakaachana nae wakiamini ni utoto tu.

Jadon Sancho

Wenzake walijiunga na timu hizo akiwemo Mshikaji wake wa damu Reiss Nelson ambaya mpaka sasa yuko Arsenal.

Watford walimpeleka katika moja ya shule mwenza iitwayo Harefield Academy ili awe anasoma wakati huo huo akicheza mpira.

Maisha yaliendelea huko mpaka mwaka 2015 alipoamua kujiunga na akademi ya Manchester City na huko ndiko alileta mapicha picha usipime.

Sancho akiitumikia Manchester City Academy

Kijana Sancho mwenye miaka 14 pale Akademi Manchester City alikua na kiwango bora kwa timu za vijana mpaka akapewa ahadi ya kupandishwa timu ya wakubwa na Raisi wa klabu hiyo bwana Khaldoon Al Mubarak ambaye ahadi hio aliitimiza baadae.

Mwaka 2017 wakati City wameshafanya mipango yote ya kwenda ‘Tour’ nchini Marekani na ticket wameshakata ghafla Sancho akawaambia hajisikii kwenda na kusema hata akienda hatocheza kwani kocha Pep Guadiola hampi nafasi na anataka kuondoka Etihad akatafute malisho mapya.

Mabosi walimshangaa kijana huyu mdogo mwenye maamuzi makubwa hivyo, walivyorejea waliongea na wazazi wa Sacho ili kuyamaliza hayo lakini Sancho mwenyewe alisema hapana na kumwambia baba yake kuwa anataka kwenda Ujerumani.

Jadon Sancho akikaribishwa Dortimund

Agost 2017 Sancho alisafiri na baba yake mpaka Ujerumani ambapo alisaini mkataba wa kuwatumikia Dortmund na katika mkataba huo akaweka kipengele cha kujumlishwa moja kwa moja kwenye timu ya wakubwa na sio Akademi tena.

Baada ya hapo gari lake liliwaka kilichofuata kila mtu anakishuhudia, na mabosi wa Dortmund wanaamini kuwa Sancho ndiye mrithi sahihi wa Ousmane Dembele aliyecheza pale kwa mafanikio kabla hajatimkia Barcelona.

Kupanga ni kuchagua, tusishangae akikataa kwenda Manchester United, Barcelona na Madrid akaenda zake Aston Villa kwa Samatta  (Utani)

Sambaza....