“AFRICA IS FOR AFRICANS … BLACK AFRICANS!”
Haya ni maneno ambayo Okello “Konga Mbandu” alimwambia rafiki yake wa toka Utoto ambae alikuwa na Asili ya Kiasia Bwana Jay “Roshan Seth” baada ya Tamko la Kufukuzwa kwa Raia wote wa Kigeni Nchini Uganda na Rais wa Wakati huo Idd Amin Dada kwenye Filamu iliyotoka mwaka 1991 na kuchezwa na Kijana wa wakati huo Denzel Washington! Filamu ambayo ilikuwa inajaribu kuelezea namna Dhambi ya Ubaguzi ilivyomea ndani ya mioyo ya Wanadamu na namna ya kuiondoa miongoni mwetu!
Kumbukumbu ya maneno hayo ilinijia mara tu baada ya kuyasikia Maneno ya Kocha wa Orlando Pirates akiongea baada ya mechi kuisha! Niseme tu hadi muda huu sijamuelewa kama yule Kocha anafaa kuwa Kocha wa Mpira ama akajiunge na vikundi vya Wanaharakati huko kwao!
Kocha anaulizwa juu ya hisia zake Kiufundi kwenye mechi anaanza na Kuwashambulia Simba SC Tanzania juu ya Mapokezi yao! Anawashambulia Simba juu ya VAR, Anawashambulia Simba juu ya Penati anawashambulia Simba juu ya Usafiri na mwisho anawashambulia Simba Juu ya Uwanja! INACHEKESHA na KUSIKITISHA kwa Kocha anaefundisha Timu Kubwa zaidi Nchini Afrika Kusini ya Orlando Pirates kutoa Cheaply Allegations mara tu baada ya kupoteza Mechi ilhali wakati alipoenda Kwenye Mkutano wa Kabla ya Mechi alisema wanafurahia kila Sekunde waliyokaa Dar es Salaam na Furaha yao itatamatika kwa Kuifunga Simba kwenye Uwanja wao!
Hebu tuanzie mbali kidogo katika huu Mjadala wetu wa Watu kutoka Afrika na Tabia zetu za Kiafrika! Timu ya Orlando Pirates ilitoa Taarifa kwa Uongozi wa @Simba SC Tanzania kwamba Watafika Alfajiri ya Jumamosi tarehe 16 milango ya Saa nane Usiku/Alfajiri lakini kwenye Mitandao yao ya Kijamii Rasmi wakaweka Taarifa za Uongo mnamo majira ya saa 4 Usiku saa Tanzania siku ya Ijumaa Saa tatu usiku saa za Afrika Kusini kwamba ndio wanaanza safari yao kuja Tanzania na Wanatarajia kufika Tanzania siku ya Jumamosi saa mbili na nusu Asubuhi siku ya Jumamosi wakipitia Nchini Kenya na kuweka Kituo pale Nairobi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mzee Jomo Kenyata!
Taarifa yao ile ilikuwa na nia gani dhidi ya Wenyeji wao ambao ndio watakaoenda kuwapokea? maana yake ni kama Walibadili ratiba yao ya Safari! Uongozi wa Simba niwapongeze hawakufanya kazi na Taarifa ile ya Instagram wakabaki kwenye taarifa yao ya kwanza kwamba wageni wao wataingia saa nane usiku/alfajiri na sio saa mbili na nusu asubuhi! Hivyo basi Kiongozi aliyeandaliwa Kuwapokea Orlando Mzee Kisiwa na Watu wake walifika uwanja wa Ndege wa JKN katika Muda muafaka na kuwasubiri Wageni wao ambao milango ya saa nane Usiku walifika!
Hii ina Maanisha Orlando waliamua kutaka kuleta Kadhia kwa Wenyeji wao ambayo walifeli Vibaya! Mzee Kisiwa na Delegation yake waliwapokea Wageni wao kwa kuwapa Zawadi kadhaa ikiwepo Korosho ambazo Wageni wale walizipokea na Ushahidi wa Picha upo!
Mzee Kisiwa na Delegation yake waliwaletea Magari mawili wageni wao Bus Kubwa la kubeba Wachezaji na Bus dogo la kubeba Viongozi Magari ambayo Orlando waliyakataa na kusema Wao walishaandaa Usafiri wao! Mtazameni Mgeni huyu! Anashangaza si eti? baada ya kuyakataa Magari yale Orlando na watu wao wakapanda kwenye Magari waliyoyaandaa wenyewe!
Orlando Pirates walipewa Ushauri wa Hotel za kukaa zilizo jirani na Uwanja wa Taifa lakino wao walisema Wameshamaliza suala la Hotel na Watafikia wanapopajua wao! Haya yote walifanya wenyewe kwa Ushirikiano wa Mwenyeji wao waliyemjua wao wenyewe huku wakipewa Msaada wa Balozi wa Afrika Kusini hapa Tanzania! Mwisho wa Siku Kocha na Timu yake wanapoteza Mechi wanaanza kurusha Shutuma kwa Sponga!
Wageni wale wamelalamikia suala la kucheleweshwa kwenda Mazoezini siku moja kabla ya mechi ila Ukweli ni kwamba walijichelewesha wenyewe! waliambia Muda wanaotakiwa Watoke Hotel kwenda Uwanjani, Barabara zikawekwa Tayari wapite lakini kwa mshangao wa Pikipiki ya Polisi muongoza Msafara muda ulipofika wakasema wana Kikao hivyo Masuala yote ya kwenda Uwanjani Yatasubiri kwanza!
Hivyo kila kitu walikuwa wanakwamisha, Timu ile Ilikuja na Chakula na Wapishi wao, Timu ile Ilikuja na Maji pamoja na Vinywaji vingine toka kwao, Timu ile ilishindwa tu kuubeba Uwanja wao wa Orlando Stadium na kuja nao kama wangeweza hilo basi yamkini wangeubeba!
MY TAKE!
Orlando Pirates ni Timu yenye jina kubwa yenye mtazamo wa Vitimu vidogo vidogo na Inaongozwa na Viongozi Wapuuzi!
1. Timu inayogomea kupita mlango Rasmi wa kuingilia Uwanjani kwa maneno ya kuambiwa kwamba wameroga Milango na wao wanaamini hii ni Timu ya Daraja la chini sana Kifikra!
2. Timu inayoingia Uwanjani na delegation yake kufanya vitendo vinavyoashiria mambo ya Shirki kama kumwaga Maji, Unga na mengine ya namna hiyo hii ni Timu ndogo!
3. Timu inayomkataa Liaison Officer kwa maneno ya mdomoni halafu ikiambiwa iandike Malalamiko Rasmi na kupeleka CAF kwamba Haimtaki Liaison Officer haiandiki ni just another street team tu kwangu!
4. Timu inayofika nchi ngeni na kukodisha Mabaunsa wa Klabu za Usiku na kuwafanya kuwa Walinzi wao hii Ni mentality ya Timu za mtaani maana kama Timu kubwa yenye kujali Weledi wangeomba Ulinzi Rasmi kutoka kwenye Vyombo Rasmi vya Ulinzi!
5. Kwenye Dunia hii ya Utandawizi na Sayansi Timu kutoka Taifa linalotajwa kuwa la daraja la Pili Duniani halafu linamnyima Chakula Liaison Officer, Afisa ambae kikanuni anapaswa kukaa kwenye Hotel waliyofikia, Kula Chakula watakachokula ili kuondosha Dhana za Tuliwekewa Sumu kwenye Chakula wao wanamzuia kwa makusudi ili tu watengeneze Agenda zao kwamba waliwekewa Sumu kwenye Chakula!
Kwa kuzingatia mambo hayo matano inatosha kukujuza namna wale jamaa kule kwao vitu Wanafanya hasa Mauaji kwa Raia wa Nchi nyingine wala sio kwa Bahati mbaya mioyo yao imejaa Ubaguzi na Chuki!
Natamani siku moja tupangiwe Mamelodi nione vile watafanya, nione vile wata behave nione namna wataingia na kutoka ili tu niweze kupata hitimisho la dhana hii dhahani kuhusu Vilabu kutoka Afrika Kusini.
Sponga Tumecheza na Al Ahly hapa Mara mbili na mara zote mbili Al Ahly walipoteza na hawakuwa na Kelele kwamba walihujumiwa, waliwekewa Sumu, walirogwa na mengine kama hayo!
Tumecheza na AS Vita Mechi nne ndani ya Miaka 3! katika Mechi ya kwanza ya Tanzania iligubikwa na Kelele nyingi za namna hii Lakini tulipoenda Kucheza nao mara nyingine Mbili tukiwafunga uwanjani Kwao (0-1) na Hapa Tanzania (4-1) Kelele hizi ziliisha na tukaambiwa AS Vita ni timu mbovu!
NB: Hawa Wachambuzi wa Mpira wa Nchi hii kila mtu ana namna yake ya kujitafutia Ugali wake! Wengine wanatafuta kwa njia za kawaida wengine wanatafuta kwa njia ya kuchafua taswira ya wengine ni kawaida hii kwenye Maisha hatuwezi kuwaza sawa hata siku moja! La Muhimu tubebe yale wanayoyasema Mazuri na yale Mabaya yasotusaidia tuwaachie wenyewe!
Tukumbuke tu AFRIKA NI YA WAAFRIKA, WAAFRIKA WEUSI kama alivyosema Bwana Okello kwenye Filamu ya Mississippi Masala!
©️Mdidi kama Mdidi the Writer😎