Sambaza....

Mkwaju wa penati wa dakika ya saba uliopigwa na kukwamishwa kambani na Djuma Shaban ulikaribia kuifanya Yanga kupate medali na kombe la ushindi lakini haikua hivyo baada ya Yanga kucheza mpaka mwisho bila bao lolote lingine.

Yanga waliingia uwanjani katika mchezo wa fainali yapili wakiwa nyuma kwa mabao mawili kwa moja baada ya kupoteza katika fainali ya mkondo wa kwanza nyumbani dhidi ya USM Algier lakini kupatikana kwa bao la mapema kulirudisha matuamaini Jangwani.

Baada ya bao la Djuma Yanga walicheza tena dakika 83 bila bao lolote wala dalili yakukaribia kupata bao na Waarabu ilipofika kipindi cha pili dhahiri walionekana kukubali na kulinda ushindi wao walioupata Jijini Dar es salaam katika mchezo wa kwanza.

USM Algier mabingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika msimu 2022/2023.

Kadri dakika zinavyokwenda wakaonekana kulinda zaidi wakicheza “Kifainali zaidi” huku pia wakisaidiwa na mashabiki wao kuwasha baruti na kupelekea kusimamishwa kwa mchezo na kupunguza kasi ya Yanga. Na hapo sasa tunaendelea kukumbushwa kutumia vyema uwanja wa nyumbani vyema.

Wakati mchezo unaendelea pengine ulitamani mchezo wa Dar ungekua umeisha kwa ileile sare ya bao moja kwa moja angalau tungekua na tumaini lakini ndio mpira maana hata Yanga nao wameshinda ugenini. Unawaza pengine Yanga wangechangamka zaidi katika mchezo wakwanza kama ambavyo ilikua jana mambo yangekua tofauti na nchi ingeingia katika historia.

Tumefungwa, tujifunze katika michezo hii ni vyema kuchanga karata zetu vyema haswa katika michezo hii inayochezwa mara mbili na zaidi ni kufanya kila linalowezekana ikibidi katika kiwanja cha nyumbani kupata matokeo.

Tuisila Kisinda akimuacha mlinzi wa USM Algier katika mchezo wa kwanza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kongole kwa kocha Nabi “master tactician” aliingia na 3:4:3 akatusuprise wote lakini tuliona matunda ya ule mfumo kwa kuwanyima Waarabu kukimbia pembeni na kupambania mpira katikati na alifanikiwa katika hilo. Kitu pekee walichomzidi Algier ni kukata mirija na kuzuia huduma kumfikia Fiston Mayele.

Hongera kwa Fiston Mayele mfungaji bora wa michuano hii pia hongera kwa Djigui Diarra kipa bora wa michuano hiyo. Historia imeandikwa kwa Tanzania na Yanga kutoa wachezaji hao bora katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika 2022/2023.

Mudathir Yahya akitaka kumdhibiti kiungo wa USM Algier.

Yanga wamecheza fainali hii baada ya miaka 30 kupita baada ya Simba kucheza mwaka 1993 kitu tunapaswa kufanya ni sasa kuzizoea fainali hizi za Afrika isitokee tena tukakaa miaka mingine mingi zaidi kama sasa. Vilabu vyetu vizoee hatua hii naamini kuna siku tutafunga mitaa tukipokea Kombe la Afrika na si haya yanyumbani tena.

Sambaza....