Kiungo wa timu ya taifa ya Croatia na klabu ya Realmadrid Luka Modric amefanikiwa kubeba tunzo ya mchezaji bora wa dunia iliyoanzishwa na gazeti la nchini Ufaransa, Ballon D’or.
Modric ambaye alifanikiwa kuingia fainali ya kombe la dunia la mwaka 2018 nchini Russia , pamoja na kubeba kombe la klabu bingwa barani Ulaya akiwa na klabu yake ya Realmadrid.
Ushindi huu unavunja utawala rasmi wa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, ambao kwa pamoja wamebadilishana tunzo hiyo wao wawili kwa miaka 10 mfululizo.
Mara ya mwisho kwa mchezaji tofauti na Cristiano Ronaldo pamoja na Lionel Messi kushinda tunzo hii ilikuwa mwaka 2007 ambapo Ricardo Kaka alibeba.
Tangu hapo Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wamekuwa wakibadilishana wao wawili.
Katika tunzo hizi, Cristiano Ronaldo amekuwa mshindi wa pili, mshindi wa tatu akiwa Antoine Griezmann ambaye alishinda kombe la dunia la mwaka 2018.
Klyane Mbappe amefanikiwa kushika nafasi ya nne, huku Lionel Messi akishika nafasi ya tano kwenye tunzo hizi.
Nafasi ya sita imeshikiriwa na Mohammed Salah, mshambuliaji ambaye aliingia kwenye rekodi ya washambuliaji wa Liverpool kama kina Roger Hunt ambayo waliwahi kumaliza msimu wakiwa na jumla ya idadi ya magoli 40.
Mfungaji huyu bora wa ligi kuu ya England, amefuatiwa na beki wa timu ya Ufaransa ambaye ni mshindi wa kombe la dunia mwaka 2018 , Raphael Varane.
Nafasi ya nane imeenda kwa Eden Hazard, huku nafasi ya Tisa ikenda kwa Kelvin DeBryune na Mshambuliaji wa Tottenham hotspurs, Harry Kane akikamilisha kumi bora ya Ballon D’or.