Simba Day 2023, Unyama Mwingi! Ni Miaka 14 ya Tamasha hili kubwa Tanzania na Afrika nzima, ndio ni mwaka wa 14 linaenda kufanyika baada ya kuanza rasmi 2009.
Moja kati ya mawazo bora sana ambayo yataendelea kuishi ndani ya Familia ya Simba Sports Club! Hapa wanatambulisha wachezaji wapya, wanacheza mechi ya kirafiki kwaajili ya mashabiki kuona wachezaji wao.
Kama kuna benchi la ufundi jipya basi wataitumia Simba Day kutambulisha na kuwapa fursa mashabiki kufahamu wahusika katika eneo hilo, hivi ndivyo Simba Day inaishi na Mashabiki zao wanaiishi.
Msimu huu Matarajio ni makubwa sana kwa mashabiki kutokana na usajili uliofanywa na benchi la ufundi lililopo! Yes, matumaini ni makubwa sana kwa mashabiki wa Simba msimu ujao.
Simba wamekaa na wamefanya usajili wa wachezaji wapya ambao wana ubora na wanaweza kutoa “backup” nzuri kama ambavyo aliomba kocha. Wamemleta Che Malone, Miquissone, Ngoma, Onana na Kramo hao ni “Quality players” kutoka nje ya nchi.
Che Malone na Onana ni MVP’s kwa walipotoka! Kramo ni mchezaji wa daraja la juu kwa Klabu na Ligi aliyotoka ( Asec Mimosas & Ivory Coast )! Ngoma ubora wake unafahamika kuanzia AS Vita mpaka pale Al Hilal, Luis Miquissone kama akiwa yule basi sio stori tena lazima atatoa kitu bora sana.
Rahisi! Naweza kusema kwamba usajili waliofanya msimu huu umekuwa mvuto sana kwa mashabiki wa Simba na kwa kiasi kikubwa inaweza kuwa chanzo cha kumaliza tiketi zao mapema yani “ALL TICKETS SOLD OUT”
Kuhusu kujaza uwanja kwao sio shida zao sababu ni jambo rahisi sana kwa Simba na Tamasha lao! Mashabiki bora sana kwa Klabu yao wapo tayari kwenda kuijaza Benjamin Mkapa Stadium.
Evodius Oscar