Wakati kikosi cha Taifa Stars kikiondoka alfajiri ya leo kuwafwata Cape Verde kwao wachezaji watatu wameachwa jijini Dar és salaam.
Kiungo wa Simba Jonas Mkude, beki wa Yanga Andrew Vicent na kiungo wa Azam FC Frank Dumayo wameachwa na kikosi cha Stars kutokana na kuwa majeruhi hivyo kushindwa kutumika katika mchezo huo wa ugenini.
Kikosi kamili cha Taifa Stars kilichoenda Cape Verde ni Aishi Manula, John Boko na Shomari Kapombe (Simba), Salum Kimenya (Prisons), David Mwantika, Abdallah Kheri, Aggrey Morris, Yahya Zaydi na Mudathir Yahya (Azam FC), Ally Abdulkarim na Paul Ngalema (Lipuli).
Wengine ni Beno Kakolanya, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Gadiel Michael, Kelvin Yondani (Yanga), Hassani Kessy (Nkana,Zambia), Abdi Banda (Baroka,Afrika Kusini). Mbwana Samatta (KRC Genk,Ubelgiji), Himid Mao (Petrojet,Misri), Simon Msuva (Al Jadida,Morocco), Rashid Mandawa (BDF,Botswana), Farid Mussa na Shabani Chilunda (Tenerife,Hispania) na Thomas Ulimwengu (Al Hilal,Sudan)