Johan Cruffy mmoja ya watu walioupa maana mchezo wa soka, akiwa kama mchezaji na pia kama Kocha, yote tunayoyaona pale Barcelona yalianzia katika kichwa hichi, alijua mpira unataka nini akaupatia, mauti yalimfika mwaka 2016 alilala bila kuamka katika kitanda chake pale Barcelona catalunya.
Kabla hajamaliza pumzi zake pale Barcelona alishawahi kutamka siri ya mafanikio akiwa uwanjani alitamka maneno machache tu, there is only one ball, so you need to have it alimaanisha kwamba kuna mpira mmoja uwanjani, hakikisha unakuwa nao, sikuelewa nini alimaanisha mpaka pale nilipomuona Gerson Fraga.
Gerson Fraga Viera mchezaji mwenye asili ya kibrazil katika uzi wa Simba, akicheza katikati ya dimba la uwanja wa taifa uchezaji wake walau unatupa maana ya maneno aliyotuachia gwiji wa soka Johan Cruffy katika ardhi yetu ya Tanzania, anajua silaha kubwa ya mchezo wa soka ni mpira wenye uzito wa gramu 450.
Kupitia yeye unaiona Simba inavyocheza katikati anajua kuituliza timu kutokana na ubunifu alionao, control zake pale anapokuwa na mpira haikufanyi kuwa na shaka kuamini ametokea nchi moja na wachezaji kama Fernandinho
Fraga technical master wa Simba uwanjani , pasi zake makini zinaifanya Simba kusogea zaidi mbele, kwa namna anavyozipiga anainua macho juu kisha anatizama wapi pasi iende taratibu anapiga kama hataki, anakufanya umtizame tena
Unyumbulifu wake wa mpira licha ya kuwa na urefu wa futi 5’11” unaridhisha pia kwa namna anavyozidi kupata nafasi ya kucheza, ana maamuzi ya haraka, anajua wapi apige wapi asipige ni mtunzi wa mipango ya Simba inayokufanya kutojutia kuitoa mia tano yako kuitizama kibanda umiza.
Ukabaji wake unanifanya kuwa na wasi wasi na damu yake, sidhani kama ana damu ya wazungu, anakaba haswa, ana ubabe ambao kiungo yoyote makini anatakiwa kuwa nao.
Kwa karibu unaziona chembembe za Claudio makelele katika miguu yake huko ubabe wake ukitukumbusha jeuri aliyokuwa nayo Gennaro Gattuso pale San Siro ulikua huwezi kuchukua mpira kirahisi rahisi.
Fraga movements zake zinamfanya kiungo anaecheza nae kurelax na kuwa mbunifu, anajua sana kucheza na timing, anarudi chini kisha anamfanya Mzamiru Yassin kucheza katika space kwa ufree, huku yeye akihakikisha anatengeneza shield cover nyuma yake.
Yote hayo yananifanya niende Brazil kwa hisia nambiwa huyu enzi akiwa mdogo alicheza timu za vijana za taifa za Brazil ngazi karibia zote timu ya under 15, under 17, na under 20, katika timu ya taifa ya under 17 alikua nahodha wao, amecheza na watu kama Douglas Costa anayecheza Juventus kwa sasa.
Akiwa kijana mdogo alianza safari yake ya soka katika klabu ya Gremio, sehemu ambayo mfalme wa soka la pasi za kuvutia Ronaldinho alipita pale mwishoni mwa miaka ya 90.
Huyo ndo Gerson Fraga Viera anaekufanya umtizame yeye kwanza kisha utizame mpira, anajua stadi za mpira haswa, soka tamu lenye uzuri wa princess diana analiweza, bado shoo za kibabe za kuchafua roho na viungo wasumbufu ni mziki mwingine.
Ukikutana nae mwambie asante kwa kukubali kuja Tanzania kwa kuja kwake, tumeona maana ya maneno ya Johan Cruffy, Asante sana Gerson Fraga Viera.
Imeaandaliwa NA MESHACK MELELE