Sambaza....

Dar es Salaam Tanzania mitaa ya Msimbazi yalipo makao ya klabu kubwa nchini ambayo ni bingwa mtetezi wa Ligi Kuu Bara Simba SC, kuna mchezaji mmoja mwenye miguu yenye Macho Matatu.  Si mwingine ni Miraji Athumani Madenge ‘Shevinshenko’.

Sheva winga ambaye katika makuzi yake alipita pale Msimbazi kabla ya kwenda kutafuta marisho kwingine na kujifua ipasawavyo na leo hii karudi kuipeprrusha bendera yenye rangi nyekundu na Nmnyeupe viwanjani.

Miraji Athumani “Sheva”

Watu wa mpira wanakwambia mchezaji anapaswa kuwa na B tatu kwa maana ya Ball Balance, Ball Brain na Ball Control, Vivyo hivyo kwa miraji na kimeongezeka kitu ambacho ni jicho la tatu.

Jicho la tatu kwa maana ukiachana na hizo B tatu, bado Sheva anauwezo mkubwa wa kunusa, kuona goli, anafunga usipotarajia ana “assist” usipotegemea.

Umri wake ni miaka 26, jamaa jicho lake la tatu limecheza na muda, miaka hiyo ndio muda mwafaka wa mcheza soka kupiga mpira mwingi kwa manufaa yake ya baadae.
Pale Msimbazi yupo mahali salama, akiwa kwenye utimamu wa mwili tutegemee kumuona akiwasha moto ipaswavyo, Ligi kuu, FA, mashindano ya Africa na hata ile michezo ya Kitaifa akiwa na uzi wa Stars.

Miraj Athumani akiwa na uzi wa Stars!

Jicho lake la tatu ndilo linampa nafasi kwenye kikosi cha watu wa kazi 11 uwanjani pale, kuwaacha mawinga zaidi ya watano nje sio kitu kidogo, na ikumbukwe wale wanaobaki benchi sio wa kawaida ni watu haswa. Katika kuthibitisha hilo mpaka sasa Sheva ana bao sita katika VPL huku akikosa michezo mingi kutokana na majeruhi.

Kila lakheri Miraji Athuman, Uwezo wako ni mkubwa pigania ndoto zako ipo siku tutakuandika kivingine chanya zaidi.

Sambaza....