Sambaza....

Kaimu kocha mkuu wa klabu ya Simba Sc Juma Mgunda amezungumza na waandishi wa habari lep kuelekea mchezo wa pili wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mgunda akiwa Bunju katika viwanja vya Mo Arena kwenye mazoezi ya timu ya Simba wakijiandaa kuikabili De Agosto ya Angola katika mchezo wa marudiano amesema wachezaji wake wanajituma na kufanya kazi na ndio maana timu inapata matokeo chanya.



“Ni kweli wachezaji wamekuwa wakifanya kazi nzuri na matokeo yanapatikana jambo ambalo tunamshukuru Mungu kwa yote,” Juma Mgunda

“Benchi la ufundi limekuwa likifanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na hasa Seleman Matola ambaye ni msaidizi huyu ni zaidi ya msaidizi kutokana na kuwa ni nguzo ya mafanikio kwenye ufundi.” Alimalizia Juma Mgunda ambae anatarajia kuiongoza Simba siku ya Jumapili mbele ya Waangola

Juma Mgunda kocha wa zamani wa Coastal Union yupo katika nafasi nzuri ya kuivusha Simba na kuipeleka katika hatua ya makundi ya Klabu bingwa Afrika baada ya kupata ushindi wa mabao matatu kwa moja ugenini.

Sambaza....