- Safari ya Yanga, Mikononi mwa Dube
- Simba na Yanga nani anaongoza kuweka mpira kwapani.
- Yanga Waweweseka! Gamondi Nje!
- Fadlu Tunaamini anawapa Ubingwa Wekundu
- Manuel Neuer ana umri sawa na uchambuzi wa soka kwa kompyuta
Kocha wa Coastal Union ya Tanga, Juma Mgunda amewapongeza Simba kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwenye mchezo wa ligi uliofanyika Jumatano ya wiki hii kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga.
Mgunda amesema licha ya kuwafahamu Simba lakini walijaribu kupunguza makosa kwenye sehemu ya ulinzi lakini haikuwa rahisi kutokana na ubora wa wachezaji wa Simba na makosa ya kujirudia rudia ambayo waliendelea kuyafanya licha ya kutangulia mapema kwa bao la Raizin Hafidh kabla ya Meddie Kagere kufunga mawili kwenye kipindi cha pili.
“Tumecheza mpira saa nane na tumemaliza salama, la pili nimekubali tumepoteza mchezo wa leo, lakini kubwa tumecheza na timu yenye wachezaji waliobora lazima tuseme ukweli, wachezaji wangu wamejitahidi kadri ya uwezo wao, na niliwaambia vijana mkicheza na watu ambao wanawazidi mkifanya makosa ya kurudia watawaadhibu, tumefanya makosa ya kurudia kwenye eneo la kujilinda na tumeadhiwa na makosa ya kimchezaji” amesema.
Hata hivyo Mgunda amesema mchezo huo umewapa la kujifunza hasa namna ya kupambana na timu kubwa zenye wachezaji kama wa Timu ya Simba na pengine huko mbeleni hakutakuwa na makosa ambayo waliyafanya kwenye mechi dhidi ya wekundu wa msimbazi.
“Lakini yote kwa yote tumejifunza katika mchezo huu, yale mazuri ambayo vijana wamejaribu kuyaonesha na yale mapungufu ambayo vijana wameyaonesha tutakwenda kuyafanyia kazi ili kuhakikisha mechi zijazo tunafanya vizuri,” amesema.
Kuhusu maendeleo ya ligi, Mgunda amesema ligi imeendelea kuwa ngumu kwa kila timu na mpaka sasa hakuna ambaye anazembea labda kutokana na nafasi aliyopo, na amesema licha ya michezo michache kubaki lakini anaamini ligi itaendelea kuwa ngumu zaidi.
“Nilisema toka awali hii ligi itakuwa ngumu watu wakasema huyu mzee anasema sema tu lakini sasa nataka niwaambieni hii ligi itakuwa ngumu mpaka mechi za mwisho, kwa sababu kuna makundi karibia matatu, kuna wanaotaka kuchukua ubingwa, kuna wanaotaka nafasi za juu, kuna wale ambao hawataki kushuka na hata huko kuna watu wanaokimbi kucheza play-off kwa hiyo ligi itakuwa ngumu zaidi huko mbeleni,” amesema.
Licha ya kichapo hicho Coastal Union hawajaondolewa kwenye kumi bora za ligi kuu wakiwa wanashika nafasi ya nane kwa alama 41 baada ya michezo 33 wakati Simba wanazidi kukisogelea kiti cha uongozi wakiwa na alama 60 kwenye nafasi ya tatu, wakizidiwa alama 14 na vinara Yanga SC ambao wao walipoteza mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar kwa bao 1-0.