Tovuti ya kandanda.co.tz kwa wiki hii yote itakuletea mahojiano ambayo imefanya na Kelvin John, mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 (Serengeti Boys). Fuatilia mfululizo wa mahojiano hayo kwa njia ya uchambuzi pekee hapa hapa katika ulimwengu wa soka, ukiletwa na mimi Martin Kiyumbi.
Tanzania kwa mara kwanza ilikuwa mwenyeji wa michuano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 Afrika,AFCON U17. Tanzania ikifanya vibaya katika michuano hiyo baada ya kupoteza micheo yote na kutoka bila ya alama na kuwa moja ya timu iliyofungwa bao nyingi.
Swali: Mashindano ya Afcon yamemalizika kipi kikubwa ulichojifunza?
Kelvin John:
“Kikubwa nilichojifunza kwenye mashindano ya AFCON, haya yalikuwa ni mashindano makubwa kuliko mashindano mengine tuliyowahi shiriki kabla. Tulishiriki CECAFA, Tukaja kushiriki COSAFA lakini ugumu wa mashindano ya AFCON huwezi kufananisha na haya mashindano mengine.”
Kabla ya kuingia katika mashindano hayo, Serengeti boys ilipata mechi za majaribio ikiwa pamoja na michuano kadhaa nchini Uturuki na Rwanda. Lakini michuano yote hii ya awali ni kama haikusaidia, Kelvin anasemaje kwenye hili suala…
Swali: Kwa hiyo inawezekana michezo mliyocheza awali haikuwa na mazoezi tosha kwenu ?
Kelvin John:
“Inawezekana kwa sababu ukiangalia mashindano tuliyoshiriki tulikutana na timu ambazo ni tofauti na timu ambazo tumekutana nazo kwenye mashindano, afu wenzetu walikuwa na nguvu sana kwenye miili yao kuliko sisi kwa sababu ya maumbo makubwa.”
Itaendelea…….