Watu wengi ni kama hawakunielewa niliposema Fiston ni wa kawaida. Yawezekana wao wanaamini kwamba mchezaji huyo ni wa zaidi ya kawaida.
Nikiwa kama mmoja wa mashabiki wa mpira wa Tanzania tangu miaka ya 1980, nimeshashuhudia washambuliaji wengi wenye kujua kufunga, siyo tu mabao, hadi shule!
Kwa kumlinganisha na huyu, narudia tena, huyu ni wa kawaida sana, siyo kama wale.
Fiston ana mabao 11 hadi sasa katika ligi yenye timu 16 huku ikiwa katika mzunguko wa 19.
Na anafuatiwa na Reliants Lusajo wa Namungo mwenye mabao 10, na George Mpole wa Geita Gold mwenye mabao 9.
Ona hawa
John Bocco wa Azam FC, msimu wa 2011/12 alifunga mabao 19 katika ligi iliyokuwa na timu 12 tu, maana yake msimu mzima ulikuwa na mechi 24…na hakucheza mechi zote!
Aliyemfuatia alikuwa Emmanuel Okwi wa Simba aliyefunga mabao 12…mind the gap!
Herry Morris Ng’onye wa Tanzania Prisons msimu wa 2002 alifunga mabao 11 katika ligi iliyokuwa na timu 8. Yaani msimu ulikiwa mechi 14 tu kwa kila timu…mwanaume katupia 11.
Mchambuzi wetu ndugu @jemedarisaid akiwa 82 Rangers, alimaliza katika nafasi ya tatu akifungana na Ulimboka Mwakingwe wa Reli ya Morogoro kwa mabao yao 5.
Msimu wa 2012/13 Kipre Tchetche wa Azam FC alifunga mabao 17 katika ligi uliyokuwa na 14, maana yake msimu mzima ulikiwa na mechi 26 kwa kila timu.
Wakati Kipre akifunga mabao 17, aliyemfuatia alikuwa Didier Kavumbagu wa Yanga aliyefunga mabao 10. Mind the gap!
Hebu ona na hawa.
1996 Mohamed Hussein (Yanga) 26
1997 John Joseph (TZ Prisons) 24
1998 Edibily Lunyamila (Yanga) 25
1999 John Thomas Masamaki (Mtibwa) 25
2006 Abdallah Juma (Mtibwa Sugar) 20
2008-09 Boniface Ambani (Yanga) 18
2009-10 Mussa Mgosi (Simba) 18
2010/11 Mrisho Ngassa (Azam) 18
2015/16 Amis Tambwe (Yanga) 21
2017/18 Emmanuel Okwi (Simba) 19
2018/19 Meddie Kagere (Simba) 23
2019/20 Meddie Kagere (Simba) 22
Nimewaona kina Joseph Kaniki Golota akizifunga timu ngumu za Waarabu, kwa Macho yangu nimemuona Felix Sunzu akifunga magoli anavyotaka hapa..
Hivi Mnamkumbuka Yule Sunguti?? Mkenya Babu aliyecheza Yanga?? Acheni wendawazimu nyie. Alikuwa anafunga bila kupasiwa na adui wa timu aliyepokea bahasha Wala any assistance from referee.
Je mnataka nimsifie Fiston kwa kuifunga Geita kwa Goli la Asante Refa??
Binafsi Nina akili zangu timamu ninazozitegemea katika utashi, kuamua, kuwaza na kuwazua…
Nikiwa na akili zangu timamu, niliwashuhudoa hawa wakicheza na kufunga mabao, narudia tena, Fiston wa kawaida sana!
Huwa namuona Kama Mwaikimba mwenye uchu tu.
Imeandikwa na Stevie Mwarabu, Shabiki wa Kandanda kutoka Iringa