Mchezo wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Rivers United dhidi ya Yanga sc umekamilika kwa timu ya Yanga kushinda magoli mawili kwa bila.
Mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Godsula Akpabio nchini Nigeria Yanga sc ilijipatia magoli yake kwa mshambuliaji raia wa Kongo Fiston Mayele katika dakika ya 73 na 81.
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilikamilika bila timu yoyote kupata goli na ikamlazimu kocha wa Yanga sc kufanya mabadiliko mwanzoni tu mwa kipindi cha pili kwa kumtoa Joyce Lomalisa na kuingia Kibwana Shomari Djuma Shaban nafasi yake ikachukululiwa na Jesus Moloko na Faridi Mussa na aliingia Tuisula Kisinda.
Mabadiliko hayo yalizaa matunda baada ya dakika ya dakika ya 73 Fiston Mayele kufunga bao la kwanza akipokea pasi kutoka kwa Bakari Mwamnyeto na dakika ya 81 Yanga sc walipata goli la pili kupitia tkwa Fiston Mayele tena baada ya kupokea pasi nyingine kutoka kwa Bakari Mwamnyeto kutokana na shambulizi la kushtukiza.
Kwa ushindi huo sasa wanakua wamelipa kisasi kwa Wanigeria hao kwani mwaka 2021 walikubali kichapo cha bao moja kwa sifuri nchini humo na sasa imebaki kurudia kisasi hicho Benjamin Mkapa kwani pia Yanga ilipoteza kwa bao moja bila.
Huo ulikuwa mchezo wa mkondo wa kwanza wa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na mkondo wa pili utachezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili.