Aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa timu ya Simba, Masoud Irambona Djuma, amepata timu nchini Rwanda kwa mkataba ambao ni ” mnono” kwa mujibu wa vyanzo vyetu.
Irambona Masoud Djuma amesaini mwaka mmoja kuinoa timu ya AS Kigali.
Ataanza kazi rasmi leo bila winga wa kushoto mrundi Emmanuel Ngama aliesajiliwa na Hull City ya Uingereza kwa kitita cha paundi 220,000.
Emmanuel Ngama 27 aliwahi kusajiliwa na Reading ya Uingereza akiwa mdogo akashindwa akarudi Afrika.
Amechezea timu za URA Uganda, AFC Leopards ya Kenya.
AS Kigali msimu uliopita walikosa ubingwa wa ligi wakiwa namba 2 kwa Apr wakakosa kombe la Amani Peace Cup kama FA Cup.
Hiyo ilisababisha kumfukuza kocha wao kiungo mkabaji namba 6 wa zamani wa Apr Masoud alikuwa kiungo namba 8 wote Apr.
Walipoifunga Simba 1-0 mechi ya kwanza Kagame Cup 1996 na kufungwa 1-0 fainali na Simba.