Imeripotiwa kuwa klabu ya Manchester United ipo katika mazungumzo na klabu moja nchini China kwa ajili ya uhamisho wa kiungo wao raia wa Ubeligiji Marouane Fellaini.
Mpaka sasa jina kamili la klabu hiyo halijawekwa wazi lakini pia uhamisho huo unaweza kufanyika muda wowote kuanzia sasa kwani dirisha la usajili la nchini China linafungwa Februari 28.
Fellaini mwenye umri wa miaka 31 alijiunga na Manchester United akiwa ni usajili wa kwanza mkubwa wa kocha David Moyes baada ya kuondoka kocha Alex Ferguson akitokea Everton kwa ada ya uhamisho wa Paundi Milioni 27.5
Toka
mwaka aliosajiliwa yaani 2013, Fellaini amekuwa si chaguo la mashabiki wa
Manchester United licha ya makocha wote watatu David Moyes, Louis Van Gaal na
Jose Mourihno wakimtumia katika mechi muhimu na anaondoka huku mkataba wake
ukiwa bado haujaisha, kwani kikomo chake ni mwaka 2020.