Sambaza....

Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara amekiri Henock Inonga Baka ni miongoni mwa wachezaji wazuri waliopo katika kikosi cha Simba hivi sasa ambacho watakwenda kukabiliana na April 30.

Manara akiongea katika kituo cha redio amesema Mcongo huyo ni mlinzi mzuri wa kati lakini shida yake anapenda sana kucheza na mashabiki.

Inonga Baka “Varane”

“Kuna wakati anafanya (Inonga Baka) jambo ili awafurahishe mashabiki, Inonga ni beki mzuri lakini sijui shida yake inakuwa ni ipi anapenda kucheza na akili za mashabiki kuliko majukumu yake, kwa beki mzuri hawezi kufanya hivyo.” Alisema Manara.

Simba na Yanga wanakwenda kukutana katika mchezo wa raundi ya pili katika NBC Premier League na Inonga Baka ni miongoni mwa nyota wanaotarajiwa kuanza katika kikosi cha Simba.

Sambaza....