Kombe la dunia ni tukio ambalo huleta hisia za watu wengi kuwa pamoja, watu hukutana kwa pamoja na kuzungumza lugha moja ambayo huwa inakuwa yenye hisia moja ambayo ni mpira.
Tangu mwaka 1930 lilipoanza kombe hili la dunia nchini Uruguay, watu wengi wamekuwa wakitamani kuweka historia ya pamoja.
Kumbukumbu nyingi hubaki vichwani mwao kila kombe la dunia linapoisha, kumbukumbu ambazo hubaki kama simulizi kwa vizazi mbalimbali.
Kumbukumbu ambazo zina matukio ya kila aina mazuri au mabaya yanayotokea nje na ndani ya uwanja.
Kuna matukio mengi sana ambayo sisi huyakumbuka virahisi yanapotokea ndani ya uwanja kwa sababu wengi huyaona na wengi macho yetu huyaelekeza huko kwa sababu shauku yetu huwa kutazama burudani inayotokea ndani ya uwanja.
Ila kuna vitu vingi nyuma ya pazia hutokea kwenye kombe la dunia, ni ngumu kwa mtu kuviona au kuvisikia kwa wingi kwa sababu vinatokea nyuma ya pazia
Wengi macho yetu huishia kwenye matukio yanatokea ndani ya uwanja, na kumbukumbu zetu hujazwa matukio ya magoli, timu kushinda au kushindwa lakini kuna matukio yanayotokea nje ya uwanja ambayo wengi watu wengi hawayajui.
Yafuatayo ni matukio saba (7) ambayo yamewahi kutokea nje ya uwanja na wengi wetu hatuyajui.
1: Mchezaji haruhusiwi kufanya tendo la ndoa kipindi cha kombe la dunia, inasemekana mchezaji humaliza nguvu nyingi anapofanya tendo la ndoa hivo makocha wengi huwa wanawafungia wachezaji wanaofanya tendo la ndoa kipindi cha kombe la dunia, na ikizingatia mashindano ya kombe la dunia hutumia muda mfupi na ratiba za mechi huwa karibu karibu hivo makocha wengi huwa wanatoa onyo kwa mchezaji anayefanya ngono kipindi hiki kwa kuhofia kupoteza nguvu nyingi kipindi hiki.
2: Dunia inakadiliwa kuwa na watu bilioni 7.05, watu bilioni 3.2 huangalia kombe la dunia ambapo ni sawa na asilimia 46% ya watu wote duniani ambapo inakaribia kuwa 50% ya watu wote duniani.
3: Kwenye kombe la dunia kuna aina Milioni 3 za bia zinazouzwa, kwenye kombe la dunia la mwaka 2010 lita 750, 000 za bia ziliuzwa , wengi wa mashabiki hujenga urafiki na undugu ambao husababisha kupata muda wa pamoja kunywa vinywaji mbalimbali kama bia ambapo ndicho kinywaji ambacho hutumiwa kwa kiasi kikubwa na mashabiki wanohudhulia kombe la dunia
4: Kombe la dunia husababisha ongezeko la kuzaliana kwenye nchi inayoandaa kombe la dunia, mfano miezi tisa baada ya kombe la dunia la mwaka 2006 nchini Ujerumani, watu walizaa kwa ongezeko la asilimia 10, na hii ni kwa sababu ya matumizi ya pombe kwenye kombe la dunia na miingiliano ya watu wa mataifa mbalimbali ambao husababisha kushamiri kwa tamaa za ngono
5:Kila timu inayoishia hatua ya makundi hulipwa dollar milioni 8, mshindi wa kombe la dunia hulipwa dollar 35 na mshindi wa pili hulipwa dollar milioni 25, kwa kifupi hakuna timu inayotoka kapa kwenye kombe la dunia.
6: Viwanja vingi vinavyojengwa kwa ajili ya kombe la dunia hujengwa nje ya mji, mfano viwanja 12 vilivyotumika kwa ajili ya kombe la dunia la mwaka 2014 vilikuwa na umbali wa 1,997 miles kutoka makao makuu ya miji iliyotumika kama mwenyeji wa kombe la dunia. Tazama viwanja vyote hapa.
7: Kombe la dunia la mwaka 2014 ndiyo lilitumia gharama kubwa sana kwenye maandilizi, ambapo lilitumia dollar za kimarekani bilioni 14.5.