1:Kuna ligi tano bora ambazo UEFA wameziweka katika daraja la juu, Ligi kuu ya Hispania (La Liga) , Ligi kuu ya England (EPL), Ligi kuu ya Ujerumani (Bundesliga) , Ligi kuu ya Ufaransa (Ligue one) na Ligi kuu ya Italy(Seria A).
Ni aghalabu sana kushuhudia ligi hizi zikitoa kila mmoja timu moja kwenye nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya, lakini msimu huu ligi nne kati ya tano zimetoa timu moja .
Mara ya mwisho kwa nusu fainali ya ligi ya mabingwa kuwa na timu kutoka England, Hispania, Ujerumani na Italy ilikuwa mwaka 1981 na bingwa alikuwa Liverpool.
2: Liverpool na As Roma walikutana katika fainali ya European Cup mwaka 1984 na Liverpool ilishinda kwa mikwaju ya penalti (4-1) baada ya mechi kumalizika kwa sare ya 1-1 katika dakika za kawaida, Liverpool ilisubiri penalti ya mwisho ya Alan Kennedy kuwapa ubingwa mbele ya As Roma
3: Gerard Houlliers alikuwa amekaa kwenye benchi akishuhudia shujaa wake Michael Owen akifunga magoli mawili dhidi ya As Roma kwenye fainali ya UEFA Cup mwaka 2001 dhidi ya As Roma katika ardhi ya Italy
4: Wakati Liverpool na As Roma wakiwa wameshawahi kukutana katika fainali ya michuano hii ya vilabu barani ulaya, lakini cha kusikitisha Bayern Munich na Real Madrid hawajawahi kukutana katika fainali na msimu huu hawatakutana tena
5: Mechi ya Real Madrid na Bayern Munich itakuwa mechi ya 23 tangu timu hizi zianze kukutana na timu zote zimefanikiwa kushinda mara 11 dhidi ya mwenzake.
6: Hii itakuwa nusu fainali ya saba kati ya Real Madrid na Bayern Munich rekodi ambayo hakuna timu ambazo zimeifikia na itakuwa mechi ya 18 katika hatua ya mtoano ya ligi ya mabingwa barani ulaya, ambapo mechi ya Real Madrid na Juventus inafuatia ikiwa na idadi ya mechi 12 katika hatua ya mtoano sawa na mechi ya Chelsea vs Barcelona
7: Kocha wa sasa wa Bayern Munich , Jupp Heynckes alifukuzwa kazi Real Madrid baada ya kuifikisha timu hiyo fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya 1998