Hii ni kutoka mezani kwa Haji Manara!
1.Ni Dhairi kwamba Groves za Juma Kaseja bado zinaishi kwenye mikono ya Aish Manula kuna safari kubwa sana kwa Nduda ili kukaa kwenye milingoti mitatu usisahau pia Nduda ni mtu hatari sana na yeye.
2.Pierre Lechantre na Masoud Djuma sina shaka kabisa na vyeti vyao vya ukocha nafikiri walihitimu kwa kiwango cha juu sana na kuna siku Asante Kwasi atacheza kama Striker wa kati na timu ikapata matokeo pia Heshima kwao hawa walimu yale yalimshinda Joseph Omong zamani licha ya kuwa timamu..
3.Kucheza kwa Mohamed Hussein pamoja na Asante Kwasi kunaufanya upande wa Kushoto kuwa na kasi sana na kunaufanya upande wa kulia pia kuwa na kasi sana ukichanganya na uwepo wa Shiza Kichuya kama kocha mwingine angeweza kuamini sub ya Asante Kwasi always ni Tshabalala lakini chini Masoud Djuma na Pierre Lechanter si hivyo tena
4.Yusuph Mlipili ni mtu muhimu zaidi pale nyuma kuliko kawaida ukichanganya na uwepo wa Erasto Nyoni na Juuko Murshid unapata ulinzi wa hali ya juu na unapata ukuta mgumu zaidi VPL ndio ni Yusuph Mlipili ambae alikuja kama sub pale Simba lakini mwisho wa siku amekuwa kiongozi pale nyuma alivyogundua muhimu ni kujituma na kujiamini basi akawa Yusuph Mlipili mwingine tofauti na Yusuph Mlipili wa Toto Africa wa kipindi kile.
5.Rahisi sana kugombania namba na Nicholas Gyan au Haruna Niyonzima lakini ni ngumu sana kujaribu kumtoa Jonas Mkude katika eneo lake kiufupi huyu ndie Master Plan wa kiungo ya kati kaka yangu Joseph Omong hakuwai kuelewa somo juu ya Jonas Mkude mtu ambaye yupo bize na kiungo ya chini hata muda wa kuchana nywele hana…ndio ni Jonas Mkude anaefanya kila kitu kuwa sawa na mipango kukamilika anavaa jezi namba 20 muda wote jezi imeloa jasho.
6.Ni muhimu sana kuwa na mchezaji kama Erasto Nyoni kwanza yeye ni muhamasishaji mkuu mpira hajaanza leo pia anaifanya kazi kwa ufasaha zaidi ile ndio tafsiri ya neno Legend kama hakuna Mwinyi Kazimoto basi Erasto Nyoni ni mchezaji muhimu ndani ya Simba Sc hasa nyakati kama hizi kuelekea ubingwa wa VPL ndio maana amekuwa sehemu ya kikosi cha Simba sana msimu huu..
7.Baada ya kuacha masihara sasa Juuko Murshid ni mpya kabisa ni kiongozi mwingine mzuri nilimuitaji Juuko Murshid kama huyu ukiachilia mbali ule usumbufu wake wa kipindi kile lakini unaanzaje kuleta masihara kwenye timu yenye mabeki zaidi ya wa 5 tena wa kati nashukuru Juuko Murshid dua zangu ulizisikia..
8.Pass za kuogopwa zaidi ndani ya Simba ni za Shiza Kichuya iwe kutokea katikati ya uwanja au pembeni Shiza Kichuya anaweza kuwa mchezaji hatari zaidi ndani ya Simba achana kwanza na Magoli ya Emanuely Okwi na John Bocco ukitaka kuiona mechi ya Simba inaendaje basi mtazame Shiza Kichuya ni bahati tu kwa Aron Kalambo lakini kulikuwa na goli mbili za Shiza Kichuya unafikiri TP Mazembe ni wajinga kumtaka huyu mchawi mfupi? ndio Shiza Kichuya
9.Hakuna raha kama kuwa na John Bocco na Emanuely Okwi kwapamoja hawa ni wauwaji wakuu muda wote wanakudhuru tu unaweza kuzui ndani ya dakika 90 lakini dakika moja tu unaweza kufungwa heshima kwao..
10.Shomali Kapombe ndio mchezaji mwenye kasi kuliko mchezaji yeyote ndani ya Simba Sc.
SIMBA NGUVU MOJA ???????