Sambaza....

Hii inamanisha kuwa, beki ya kushoto ndio ina shida zaidi kwa sasa kuliko beki ya kulia… hili tutalichimba vizuri mbele acha sasa tutazame eneo la kiungo.

Katika nafasi hii, Simba imewaongeza wachezaji wawili ambao ni winga Benard Morrison, anayejua kuchekecha eneo la kulia na kushoto, ana kasi ya kufa mtu na uwezo mkubwa wa kucheka na nyavu lakini pia imemnasa Larry Bwalya, ambaye ni mrefu na mwembamba akitumia guu la kushoto. Huyu ni kiungo wa kati lakini pia anaweza kucheza kama kiungo wa ulinzi na ushambuliaji..hii inamaanisha jamaa ni Box to box midfielder.

Wote wawili wAnaungana na na  Ibrahimu Ajibu, Clatus Chama, Luis Miquissone,Francis Kahata, Jonas mkude, Fraga Vieira,Mzamiru yassin,Miraji Athumani, Said Ndemla na Hassain Dilunga kulitawala eneo la kati.

Clatous Chama

Viungo hawa 12 ndio wachezaji muhimu sana kwa Simba kwani wao ndio wanaibeba falsafa ya Simba mabegani mwao. Viungo hawa wamegawanyika katika sehemu tatu, kuna wale wanaweza kucheza kama Viungo wa ulinzi na wengine kama viungo wa kati na ushambuliaji, na kundi la mwisho ni wale wanaocheza kama viungo wa pembeni yaani mawinga.

Niambie kati ya hao kuna mmoja ana mwili kama wa Paschal Wawa? Hayupo…Acha tuchimbe hapa kidogo…

Kimataifa Simba itakutana na vigogo wa Afrika kama Al ahly ambao wao katika eneo la kati wana Amr Al Sulaya, Hamdi Fathi, Mohammed Afsha,Ahmed El Sheikh na Aliou Dieng, Momen Zacharia, Karim Walid, Nasser Maher, Hossam Ashour, Saleh Gomaa na wengine kibao, niambie unawaonaje maumbo yao..

Watakutana pia na TP Mazembe ambao wana viungo kama Christian Koffi, Glody Likonza, Rainford Kalaba, Tresor Mputu, Miche Mika, Jean Vital Ourega na wengine kibao ambao wote wana body Fitnes ya hali ya juu.

Ukichukua timu zote zilizofika nusu fainali msimu huu 2019/20 klabu bingwa Afrika, yaani Raja Club Athletic, Zamalek, Wydad Casablanca na Al ahly utabaini kuwa timu zote zina aina moja ya wachezaji katika eneo la kati. Kwanza miili yao ni mikubwa, pili ni wenye nguvu nyingi na uwezo wa kukaa na mpira mguuni bila kupokonywa.

Kuwana wachezaji wa aina hii ni uhakika kuwa mipira yote ya hamsini kwa hasini lazima washinde wao, mipira yote ya one against one, ni lazima washinde wao, eneo la kati ni lazima walitawale wao.

Haya yote yataizuia timu pinzani kutengeneza nafasi kupitia kati, badala yake wao ndio watakuwa na uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi kupitia eneo la kati.

Turudi kwa Simba, ukiwatazama wachezaji wote wa kati, utabaini kuwakati ya viungo 12, ni wawili tu wenye japo msuli, Jonas Mkude na Fraga, lakini pia nao ni wazito kweli kweli kiasi cha kuwa ni rahisi kupokonywa mpira baada ya kuzongwa na wachezaji wawili. wengine kama  Mzamiru  Yasin na Said Ndemla  wako nusu nusu, huku wote waliobakia akina Chama, Morrison na Miquissone hawa sio wakabaji, wao ni wazuri wakiwa na mpira mguuni tu.


Soma zaidi


Sambaza....