Mabingwa wa soka Tanzania bara, Yanga sc, imepangwa kundi D lenye timu za Gor Mahia ya Kenya, Rayon Sports ya Rwanda na USM Arger ya Algeria katika hatua ya 16, bora ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Droo hiyo iliyopangwa leo mjini Cairo, Misri, kundi A linajuisha timu za Asec Mimosas ya Ivory Coast, Raja Casablanca ya Morocco, AS Vita ya DRC na Aduara Stars ya Ghana
Kundi B linaundwa na timu za Al Masry ya Misri, RS Berkane ya Morocco, El Hilal ya Sudan na UD Songo ya Msumbiji
Kundi C lina timu za CARA ya Kongo, Enyimba ya Nigeria, FC Djoliba ya Mali na Williamsiville Athletic Club ya Ivory coast
Droo hiyo iliyoongozwa na Katibu mkuu wa CAF, Amry Fahmy na msaidizi wake Antony Bafoe, Yanga itaanzia ugenini hatua ya makundi kwa kuvaana na USM Arger nchini Algeria Mei 6, kabla ya kucheza na Rayon sports mjini Dar es salaam Mei 16, na itakamilisha mzunguuko wa kwanza kwa kuwafata Gor Mahia mjini Nairobi Julai 18
Mzunguuko wa pili Yanga itaanzia nyumbani Julai 29, ikiwakaribisha Gor Mahia, kabla ya kuwakaribisha USM Arger Agost 19, na kumalizia ugenini dhidi ya Rayon Agost 29