Sambaza....

NAHODHA wa Simba SC, John Bocco aliondoshwa uwanjani kwa kadi nyekundu inayoweza kumfanya afungiwe michezo mitano ya ligi kuu, lakini magoli yake mawili katika ushindi wa Simba dhidi ya Mwadui FC katika uwanja wa Kambarage, Shnyanga jana Jumapili yametengeneza historia ya kupenda katika ligi kuu Tanzania Bara.


>>>Takwimu za Bocco


 

Akiwa katika msimu wake wa kumi wa ligi kuu ‘muongo mmoja’ Bocco-mfungaji bora wa muda wote wa Azam FC amefanikiwa kufikisha jumla ya magoli 100 ( wastani wa magoli kumi kila msimu) namba 9 huyu mwenye uwezo mkubwa wa kumalizia nafasi anazotengeneza, mpigaji mzuri wa mpira wa kichwa na mfungaji anayejiamini katika mikwaju ya penalty amefikisha idadi hiyo ya magoli huku mkononi akiwa na mataji mawili ya ligi ( 2013/14 AKIWA Azam FC na 2017/18 akiwa Simba-mataji yote akishinda akiwa nahodha wa vikosi)


Si hivyo tu Bocco ana medali nne za mshindi wa pili ( 2011/12, 2012/13, 2014/15 na 2015/16 akiwa Azam FC), tuzo moja binafsi ya ligi mfungaji bora wa ligi kuu ( 2010/11) na ile ya mchezaji bora wa msimu ( 2017/18). Kwa hakika Bocco anastahili kupewa sifa na ingependeza kama Shirikisho la Soka nchini-TFF likaanza kuifadha rekodi kama hizi ili ziendelezwe.

Nani mchezaji aliyecheza michezo mingi zaidi ya ligi kuu? Inawezekana ni nahodha wa Kagera Sugar FC, George Kavila ama nahodha wa KMC golikipa Juma Kaseja ama pengine ni nahodha wa Mtibwa Sugar FC, Shaaban Nditti, lakini ziko wapi takwimu rasmi? Je, TFF haiwezi kukusanya takwimu kama hizi katika nyakati hizi za sayansi na teknolojia?

Image result for john bocco

Historia huwekwa ili kuvunjwa na inapendeza sana kuona mchezaji Fulani akifukuzia rekodi Fulani ili aivunje. Bocco ni wa kizazi cha sasa na ni kizazi hiki ambacho kimekuwa kikihifadhi takwimu na mwisho wa siku mambo yakawa mazuri kama hivi. Je, hatuwezi kuwatumia vijana wa sasa kufuatilia kwa uchunguzi yakinifu ili kufahamu mchezaji aliyejifunga zaidi katika ligi kuu yetu? Ni ngumu lakini kizazi cha sasa kinaweza kufanya kazi hiyo kama kitaaminiwa na kuwezseshwa kufanya kazi yao.

TFF itumie rekodi ya Bocco kujifunza zaidi na kuona umuhimu wa kuhifadhi kumbukumbu na takwimu binafsi za wachezaji na ligi kuu ili twende kisasa. Hongera sana Bocco kwa magoli yako 100 ligi kuu, naamini yatawafunza zaidi TFF na kuwakumbusha kazi zao za msingi katika dunia ya kisasa.

Sambaza....