Shirikisho la kandanda Barani Afrika limeufungia michezo mitatu uwanja wa Manispaa wa Mahamasina pamoja na kulitoza Shirikisho la Soka nchini Madagascar Faini ya shilingi 22,834,267 kufuatia vurugu zilizosababisha kifo cha mtu mmoja Septemba 9 mwaka huu.
CAF imefikia hatua hiyo baada ya kutokea vurugu wakati Mashabiki wakitaka kuingia kwa nguvu kwenye mchezo wa kufuzu fainali za Mataifa Afrika kati ya Madagascar na Senegal mchezo ambao uliisha kwa sare ya 2-2.
Taarifa za awali za tukio hilo, zilisema watu takribani 40 waliliripotiwa kuumia vibaya kabla ya mchezo huo kwenye mji wa Antananarivo, Ambapo uwezo wa kubeba mashabiki ni takribani watu 22,000 lakini masaa machache kabla ya mchezo huo idadi ya watu wengi walikuwa tayari wameshaingia uwanjani Huku mamia wengiwe wakiwa nje wakilazimisha kuingia ndani ya Dimba.
“Baada ya michezo mitatu ya kimataifa, Madagascar wataruhusiwa kuendelea kutumia uwanja huo,” Rais wa CAF na Madagascar Ahmed Ahmed amesema baada ya kamati Tendaji ya CAF kufanya Maamuzi hayo Jumamosi ya Jana katika Mji wa Sharm El-Sheikh nchini Misri.
Afrika kumekuwa na matukio ya watu Kufariki uwanjani kutokana vurugu, tukio kubwa zaidi kuwahi kuripotiwa ni lile la mwaka 2001 Ambapo mashabiki 127 walifariki kwenye uwanja wa Accra Sports nchini Ghana wakati wa mchezo Wa Heart of Oak dhidi ya Asante Kotoko.
Pia Mwaka 2012 watu 74 walifariki baada ya Mashabiki wa Al Masry walipoanzisha vurugu dhidi ya Mashabiki wa Al Ahly kwenye uwanja wa Port Said nchini Misri.