Sambaza....

Kwa mara ya kwanza toka mashindano ya kombe la dunia yalipoasisiwa mwaka 1991, nchi tisa wanachama wa Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA wameomba kuandaa mashindano hayo kwa mwaka 2023.

Tayari nchi za Argentina, Australia, Bolivia, Brazil, Colombia, Japan, New Zealand na Afrika Kusini wameomba kuwa wenyeji huku nchi za Korea Kaskazini na Kusini zikipanga kuomba kuandaa kwa pamoja.

Hata hivyo FIFA imewaomba wanachama wake ambao bado wanatamani kutuma maombi ya kuandaa mashindano hayo kutuma mapema kabla ya Aprili 16 ambapo ndio itakuwa mwisho kuomba uwenyeji wa mashindano hayo.

“FIFA watafanya mchakato wa wazi na usawa, ambao utahusisha tathimini ya wazi na kulenga zaidi katika uwajibikaji na haki za binadamu kwa wale wote walioleta maombi, matokeo ya kila kura za wajumbe wa FIFA zitaweka wazi,” taarifa ya FIFA imesema.

Mwaka huu michuano ya kombe la dunia itafanyika nchini Ufaransa kuanzia Juni 7 hadi Julai 7 ambapo Tanzania tulishindwa kufuzu baada ya timu ya Taifa kuondolewa katika hatua za awali za kufuzu.

Sambaza....