Sambaza....

Klabu ya soka ya Lipuli fc “Wanapaluhengo” kutoka Iringa imezidi kujiweka katika mazingira magumu katika Ligi Kuu Bara baada ya leo kupoteza katika uwanja wao wa nyumbani.

Lipuli fc ambayo leo ilikua katika dimba lao la nyumbani la Samora wakiikaribisha Kagera Sugar wamekubali kipigo nyumbani mbele ya mashabiki wao, baada ya kufungwa bao moja kwa sifuri.

Licha ya kutengeneza nafasi nyingi za mabao lakini Lipuli walishindwa kuzitumia haswa katika katika kipindi cha kwanza. Washambuliaji wa Lipuli wakiongozwa na Paul Nonga walikosa umakini kwa kushindwa kutumia nafasi hizo.

Alikua ni Selemani Mangoma “Selle Bobo” katika dakika ya 61 baada ya kupokea pasi safi ya “kisigino” kutoka kwa Edward Christopher aliachia shuti kali lililomshinda mlinda lango wa Lipuli fc.

Kwa matokeo hayo yanaifanya Lipuli fc kupoteza mchezo kwa mara ya kwanza wakiwa katika dimba lao lá nyumbani lá Samora.

Sambaza....