Sambaza....

 

Baada ya mtandao huu kuripoti tetesi za beki kisiki wa KCB ya Kenya kutakiwa na Simba SC ya Tanzania kwenye dirisha lijalo la usajili kama sehemu ya kuimarisha kikosi cha mabingwa hao wa Tanzania , beki huyo amezidi kufunga vingi kuhusu yeye pamoja na mpira wa Kenya.

Beki huyo amesema zile tetesi za kwamba mpaka sasa hivi ameshamalizana na klabu ya Simba SC ya Tanzania ni tetesi ambazo hazina ukweli wowote kwa sababu hawajamalizana na Simba SC .

“Bado hatujakaa tukamalizana na Simba SC mpaka sasa hivi , hakuna mazungumzo yoyote ambayo yamefanyika kati yetu mpaka sasa hivi kwa hiyo hakuna mkataba niliosaini na Simba SC”.

Kuhusu tofauti ya ligi kuu ya Tanzania na ligi kuu ya Kenya , Michael Kibwage amesema ligi ya Tanzania ni bora kuzidi ligi kuu ya Kenya hivo siyo rahisi yeye kukataa kuja kucheza ligi ya Tanzania .

“Ligi kuu ya Tanzania ni bora kuliko ligi kuu ya Kenya , siwezi kukataa kama nikihitajika kuja kucheza katika ligi kuu ya Tanzania kwa sasa . Hata wingi wa ushabiki ligi kuu ya Tanzania ina mashabiki wengi na inafuatiliwa sana kuzidi ligi kuu ya Kenya”.

Michael Kibwate

Pia Michael Kibwage amedai kuwa ligi kuu ya Tanzania ina wadhamini ukilinganisha na ligi kuu ya Kenya ambayo haina wadhamini hali ambayo inasababisha ukata kwenye timu za ligi kuu ya Kenya.

” Ligi kuu ya Tanzania ina wadhamini kwa sasa tofauti na ligi kuu ya Kenya. Ligi kuu ya Kenya ina ukata wa pesa tofauti na mwanzo ambapo tulikuwa tunawadhamini na tulikuwa tunapata pesa nyingi hata ya kupeleka nyumbani”- alimalizia mchezaji huyo nyota wa timu ya taifa ya Kenya , Harambee Stars ambaye pia ni nahodha wa KCB.

Sambaza....