Katika harakati za kuwania kufuzu kucheza mashindano ya bara la Ulaya kwa ngazi ya mataifa, kikosi cha wachezaji 24 cha Ufaransa chini ya kocha Didier Deschamps kimetangazwa hii leo.
Kikosi hicho kimesheheni nyota mbalimbali lakini, kuachwa kwa mshambuliaji wa klabu ya Arsenal ya Uingereza, Alexandre Lacazette na beki nguli wa Manchester City, Aymeric Laporte kumeleta mjadala miongoni mwa wadau wa soka duniani hasa kutokana na viwango walivyovionyesha msimu huu wakiwa na timu zao.
Lacazette ambaye ameionyesha kiwango poa akiwa na Arsenal mimu huu tayari ameshaweka kambani magoli 14. Wengi wanauliza kwanini mshambuliaji wa Chelsea, Olivier Giroud amejuishwa kwenye kikosi hicho huku Lacazette, Laporte na Ben Yedder wakiachwa nje licha ya kuwa na viwango vizuri?
Kikosi kamili kilichoitwa na kocha Didier Deschamps kinajumuisha magolikipa : Alphonse Areola, Hugo Lloris na Steve Mandanda.
Mabeki: Lucas Digne, Presnel Kimpembe, Layvin Kurzawa, Benjamin Pavard, Djibril Sidibe, Raphael Varane, Samuel Umtiti, Kurt Zouma.
Viungo: N’golo Kante, Blaise Matuidi, Tanguy Ndombele, Paul Pogba na Moussa Sissoko.
Washambuliaji: Kingsley Coman, Nabil Fekir, Olivier Giroud, Antoine Griezmann, Anthony Martial, Kylian Mbappe, Florian Thauvin.