Kipindi cha mapumziko ya Kimataifa Ligi karibia zote ulimwenguni husimama kupisha kalenda ya FIFA kupisha michezo ya timu za Taifa. Hiki hua ni kipindi ambacho ligi zimesimama na wachezaji wachache teuliwa hujiunga na timu zao za Taifa na kuwaacha wengine vilabuni.
Baadhi ya vilabu huamua kuendelea na programu za mazoezi na ratiba zao za kila siku lakini baadhi yao huamua kucheza mechi za kirafiki kulingana na ratiba za kambi na kiasi cha muda wa mapumziko ya Kimataifa kwani wachezaji wanaobaki katika vilabu hujikuta wakifanya mazoezi pekee pasina mechi za ushindani za kuwaweka fiti.
Katika mapumziko haya ya Kimataifa kuzipisha timu za Taifa kucheza michezo ya kufuzu AFCON pale Ivory Coast mapema mwakani, vilabu vimeendelea na kambi zao na kucheza michezo ya kirafiki.
Timu ya Simba ni moja ya timu zilizocheza michezo kadhaa ya kirafiki ikiwa ni kampeni ya kujiweka sawa kujiwinda na mashindano ya ligi kuu NBC pamoja na mashindano ya kimataifa watakayoanza kutimua vumbi Septemba 16 mwaka huu dhidi ya Power Dynamos ya Zambia.
Simba walicheza dhidi ya Kipanga na kuibuka na ushindi wa goli tatu bila, kisha wakacheza dhidi ya Cosmopolitan ya jijini Dar es salaam na kuibuka na ushindi mnono wa goli tano kwa moja na kisha wakacheza dhidi ya Ngome Fc ya jijini Dar es salaam na kuibuka na ushindi wa magoli sita bila.
Katika michezo yote hiyo ambayo Simba ameicheza, amefanikiwa kushinda michezo yote na kufunga idadi kubwa ya magoli. Lakini mtu wa soka anaweza hoji, mpenzi wa soka anaweza uliza au hata mnazi wa soka anaweza uliza kuwa, Je hizi mechi wanazocheza Simba dhidi ya timu ndogo ni sawa ukilinganisha na mashindano wanayoshiriki? Je Hiki ni kipimo tosha kwa Simba kufanya vizuri kimataifa?
Simba anapambana na timu kubwa Afrika ukilinganisha na hizi anazocheza nazo je huoni Kama Simba wanafanya mchezo wa kuigiza? Ni sawa mtu anaweza hoji vyovyote au hata kwanamna yoyote kadiri itakavyomfaa.
Lakini KANDANDA.CO.TZ ipo hapa kwa ajili ya kumaliza utata na ugumu ambao shabiki anaupata pengine anajiuliza kwanini, mwingine hata akapata wasiwasi na timu yake pengine anayo hofu ya kutofanya vizuri kitaifa na kimataifa, basi KANDANDA.CO.TZ iko hapa kukutoa mashaka yote, kulingana na sababu zifuatazo ambazo Simba wamezizingataia katika uteuzi wa michezo ya kirafiki katika kipindi hiki cha mapumzkiko ya kimataifa watakwenda kufaidika kama ifuatavyo;
● Kocha kupata nafasi ya Kuchunguza na kujua uwezo wa wachezaji.
Kabla ya ligi kuanza Simba waliweka kambi Uturuki ili kujiandaa na mashindano ya msimu wa 2023/24. Changamoto waliyokutana nayo ni kuwa timu haikusafiri yote bali waliondoka kwa mafungu lakini pia kocha mkuu aliiacha timu kambini Uturuki ikiwa chini ya kocha msaidizi na kwenda kwao Brazil kusoma kozi ya mda mfupi, hivyo kocha hakupata mda mwingi wa kuchunguza uwezo wa wachezaji wake wote kikamilifu.
Isitoshe mechi zenye uzani mdogo kama hizi ambazo hazina presha humfanya mchezaji ajiamini na kujitoa kwa kiasi chake chote na uwezo wake wote na hapo kocha anapata nafasi ya kuuona uwezo wa wachezaji wake.
● Kurudisha na kuongeza hali ya kujiamini.
Wapo baadhi ya wachezaji wamepoteza uwezo wao wa kujiamini kwa kiasi kutokana na sababu kadhaa zikiwemo majeraha na kukaa benchi kwa muda mrefu. Kucheza mechi nyepesi kiasi zisizo na ushindani mkubwa huwafanya wachezaji kujiamini. Lakini pia kwa wale waliokuwa majeruhi wanapata nafasi ya kuongeza utimamu wa mwili kidogo kidogo.
Hii ni tofauti kama Simba wangecheza na timu yenye uzani mkubwa. Lakini timu inaposhinda wachezaji hupata morali ya kutaka kuendelea kushinda katika mechi zinazofuata tofauti na kucheza na timu kubwa kisha wakafungwa kwa kiasi ingewafanya wachezaji kukosa kujiamini.
●
Mitihani au mazoezi mepesi humfanya mwanafunzi aelewe somo vizuri. Mechi nyepesi na zisizo na presha ambazo Simba wamecheza zinamsaidia kocha kupandikiza mbinu na mifumo yake kwa wachezaji kwani wachezaji hawana presha ya mchezo hivyo maelekezo na maagizo hueleweka vymema na kufanyika ipasavyo kiasi kwamba katika hizo mechi walizocheza wameibuka na ushindi mkubwa, hii ni ishara ya mbinu na mifumo ya kocha kueleweka vema.
NB: UKINUNA UWE NA SABABU.