Sambaza....

Klabu ya Yanga inaendelea na usajili wake wa kujiimarisha zaidi kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara. Mpaka kufikia jana klabu ya Yanga ilidhibitisha kumsajili Gift Mauya kutoka katika klabu ya Kagera Sugar.

Yanga mpaka sasa hivi inaendelea na usajili wa wachezaji ambao wanaonekana ni nyota na ambao watakuwa na msaada mkubwa ndani ya klabu hiyo. Mpaka sasa hivi Yanga imekuwa ikihusishwa na wachezaji wengi nyota.

Katika mazungumzo maalumu yaliyofanyika kati ya makamu mwenyekiti wa klabu hiyo ya Yanga na mtandao huu wa kandanda.co.tz, makamu mwenyekiti amewataka mashabiki wa Yanga wawe watulivu.

-Tupo imara na makini sana kuelekea kwenye dirisha la usajili, tunataka kurejesha ile heshima ya mataji tuliyoipoteza kwa muda mrefu. Mashabiki na wanachama wanachotakiwa kuwanacho ni utulivu tu”- alisema Fredrick Mwakalebela makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga.

Fredrick Mwakalebela amedai kuwa usajili huu utarudisha hadhi ya klabu ya Yanga na hivo msimu ujao watani wao wa jadi ambao ni Simba hawatokuwa na nafasi tena ya kubeba kombe la ligi kuu Tanzania bara.

Sambaza....