Sambaza....

Simba wameonekana kusajili timu imara msimu huu. Mpaka sasa wameshashusha vyuma vya maana. Good.

Miongoni mwa sehemu wanayotakiwa kufanya usajili wa maana ni katika eneo lao la golini. Hapa ni peupe.

Ni ngumu kushinda kikombe ukiwa hauna kipa imara anayeweza kukupa pointi 15 yeye binafsi katika msimu mmoja.

Hizi ni kazi za Aishi Manula. Mara nyingi Manula ameibeba Simba SC katika mabega yake. Manula atakosekana kwa muda.

Aishi Manula “Air Manula” 

Mpaka Manula arejee kiwanjani, Simba SC wanapaswa kuwa na mtu kweli langoni. Moja ya mafanikio makubwa ya Yanga katika lango lao wana Djigui Diarra.

Diarra amewapa uimara na utulivu mkubwa langoni. Katika muda huu ambao Manula atakuwa nje, lango la Simba SC linatakiwa kuwa na Mwanaume sio mvulana tena.

Kipa imara anakupa utulivu. Anakupa pointi. Anakupa kujiamini. Kipa wa timu aina ya Simba SC anatakiwa kuwa mtu imara na madhubuti sio (Saidia fundi).

Makipa walioko kambini Uturuki na timu,
Ferouz Teru na mwenzake Ally Salim wana mengi ya kujifunza kabla ya kuaminiwa kusimama katika lango la Simba SC.

Ugua pole Aishi Manula “Air Manula”

Sambaza....