Sambaza....

Kuna minong’ono mingi Sana mitaani kuhusu timu kupewa Motisha ya million 10 ikitoa sare au ikiifunga Simba. Na fedha hizi zilianza msimu uliopita tena kiwango na idadi ya fedha inayotajwa ni Ile Ile Kwa Kila timu.

Hakuna Mashaka anayetoa hizo fedha ni mtu mmoja ila anazipitisha mlango wa nyuma.

JE NI TATIZO?

Kwangu sio tatizo na halina madhara yoyote kwenye mchezo. Timu kuahidiwa fedha au kupewa kabisa ili ijipambanie nafsi yake kwa nini iwe tatizo? Lingekuwa tatizo kama timu ingekuwa inacheza chini ya kiwango Ili ipoteze mchezo.

Lakini kama ni Ili ipambane kwa ari zaidi uwanjani ishinde mechi kwangu hilo sio tatizo kabisa bali ni jambo jema linalostahili kuigwa.

Sina hakika kama ni kweli ila kama ni kweli timu zinazoahidiwa pia huwa zinalegezwa Ili zikikutana na watoa Motisha zilegeze na kucheza chini ya kiwango Ili watoa Motisha wafaidike basi hili ni tatizo na linaondoa kabisa ubora wa jambo lenyewe na tafsiri yake inageuka kuwa Sio Motisha tena bali rushwa ya kupanga matokeo.

Sina hakika kama hili lipo lakini linasemwa. Kwangu kutoa Motisha Kwa timu yoyote ishinde mechi ni jambo jema la kupongezwa.

Watoa Motisha msiishie tu kutoa Kwa timu zikicheza na Simba tu. Wapeni wakicheza na Kila timu usipokuwa wanapokutana na Nyie tu.

Mashabiki wa Simba acheni kulialia kuhusu hili. Kwanza linawaimarisha kushindana uwanjani na Kila mechi kweni inakuwa fainali. Itawasaidia wachezaji wenu kuwa imara na tayari Kwa ushindani hasa Kimataifa. Mechi dhaufu na lege lege huzaa wachezaji dhaifu na lege lege wanaoamini tutashinda tu hata bila kupambana.

Kubalini kukutana na timu zilizopewa Motisha Ili mpambane kisawasawa na mkishinda mjivune kushinda Kwa nguvu na uwezo uwanjani.

Tunaomba watoa Motisha waongeze dau ifike angalau million 60 Kwa Kila timu itakayoifunga Simba. Angalau timu iliyopewa Motisha watajua donge ni nono na watafia uwanjani Ili waifunge Simba. Na Simba ikishinda mechi nyingi kama hizo itakuwa inapitia kipimo kizuri Cha tanuru la moto tayari kwenda kupambana Kimataifa.

MOTISHA NI JAMBO ZURI NA LINAONGEZA USHINDANI. WATOA MOTISHA ONGEZENI DAU.

Jicho la tatu la Mgalilaya kutoka Facebook

Sambaza....