Anaandika Omar Kombo
Petro Atletico imefanikiwa kuingia nusu fainali ya Klabu Bingwa Afrika kwa kumtoa Mamelods Sundown sio kwa bahati ni kwasababu walijipanga, ni kwasababu bajeti yao wakati msimu unaanza ilikuwa ni shilingi bilioni 23.1.
Pia Rais wa klabu hiyo Tomas Faria wakati anaingia madarakani aliweka malengo haya.
Ndani ya kipindi cha miaka minne kutoka mwaka 2020 -2024 Petro Atletico iwe kwenye top five ya vilabu bora barani Africa na ikiwezekana kuwa klabu kubwa kuliko zote barani Africa.
Kutoka mwaka 2020-2024 asilimia ishirini ya mapato ya klabu yawe yametokana shughuli za moja kwa moja za klabu(direct operations).
Kuhakikisha malengo hayo yanafanikiwa rais wa klabu ya Petro Atletico Tomas Faria alisaini dili la miaka miwili na watu wa La Liga kwenye masula ya ushauri na mafunzo.
Kimsingi La Liga wanachokifanya ni kutoa ushauri na mafunzo kwenye maeneo haya.
Commercial and Makerting structure of club, Data and Fan engagement Management na Bussiness Development.
Haya yote yanafanyika ni kuitengeneza Petro Atletico kuwa klabu ya kisasa ili iweze kuongeza mapato na kuwa na nguvu ya kushindana kwenye club bingwa ya Africa.
NB: Kuna lakujifunza kwa vilabu vyetu.