Miaka 20 sasa tangu timu ya Mtibwa ijitambulishe vyema kwenye soka la Tanzania kwa kuja na Surprise ya ubingwa, na si ubingwa wa kubahatisha ubingwa miaka miwili mfululizo 1999 na 2000 (back to back). Kwa kutwaa ubingwa huu ulikuja na kuleta upinzani wa hali ya juu kwa vilabu vikongwe Simba na Yanga .
Kwanini Mtibwa aliweza kutwaa ubingwa back to back?
Eneo la kwanza alijikita kwenye usajili wa wachezaji bora na wakubwa (quality). Alianza kwa kubattle sokoni na vilabu vyenyewe atajavyokuja kushindana navyo kwenye ligi. Alivipora wachezaji wenye majina na performance nzuri. Wengi wanakumbuka zama zile wachezaji wakubwa wenye majina ndani ya Simba na Yanga walivikacha vilabu vyao wakaenda kujiunga na Mtibwa. Wachezaji hao ni Alphonce Modest, Monja Liseki, Shabani Ramadhan, Dua Saidi, Ally Yusuph Tigana na Mtwa Kihwelo kwa uchache.
Kwanini Matokeo ya Mchezo wao dhidi ya Simba haukihitaji Darubini kuona nani anakwenda kushinda mchezo wenyewe? Majibu ya moja kwa moja kwamba Simba alionekana kwa macho tu (naked eyes) anakwenda kushinda mchezo. Kabla ya kuzama kwa kina kwenye mifumo ya kucheza na matokeo kiujumla tuangalie vikosi vyote viwili (quality) kisha tuanzie kulinganisha hapo ,nani alipaswa kushinda kwa kigezo cha mchezaji mojamoja kabla ya kugusa ubora na uzoefu wa bench la ufundi
Wapwa zangu sitaki na sipendi kufananisha kiwango (quality) ya mchezaji moja moja, kwenye first eleven hapo nikuachie home work wewe binafsi, Mimi niguse kwa uchache hao sub 7 wa Simba ni wachexaji wa timu ya Taifa kwa asilimia 90 ambao hawajapata nafasi kwenye kikosi cha kwanza. Nikasema kimoyomoyo kama wangekuwa upande wa Mtibwa lazima wangeanza na kama wangeanza mechi ingekuwaje? matokeo yangeisha vip? Resistance( ukinzani) ndani ya uwanja ungekuwaje?
Wapwa zangu binafsi niliona kama Mtibwa kaugeukia ukweli mapema kwamba mechi ipo juu yake Thanks God milingotini kulikuwa na mtu, mtu kweli Shabani Kado ambaye kwangu Mimi yeye ndio alikuwa nyota ya mchezo incredible save za kutosha ,one against one za kutosha.
Baada ya utofauti mkubwa wa ubora na uzoefu wa mchezaji moja moja dhidi ya mwenzake katika vikosi viwili hivi, Kwa Mtibwa kulihitaji mbinu nyingi bora toka benchi la ufundi kama silaha kuweza kupata matokeo. Kuwategemea moja kwa moja wachezaji ndani utofauti ulikuwa mkubwa wa viwango. Maana wapwa zangu kadri Muda ulivyokuwa unakwenda vitu kadha vya kiufundi vilikuwa vinapungua, iliyopelekea makosa ya kiufundi ya mara kwa mara.
Je nini ukombozi wa Mtibwa kurejea kwenye ‘chart’ yao ya miaka ya 2000 kuukubali ukweli maeneo mawili; Moja: Aina ya usajili wao kugharamia na kubattle Sokoni wakati wa usajili. Pili: Kujionyesja kama timu ya wakazi wa Morogoro si ya kiwanda cha Mtibwa tu, maana yangu kushirikisha wadau wapya ambao wataguswa na mafanikio ya kimkoa zaidi.