Kuelekea mchezo wa kufuzu Afcon kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” dhidi ya Uganda “The Cranes” msemaji wa Shirikisho la soka nchini TFF Cliford Ndimbo ameendesha harambee yakununua tiketi kwaajili ya mashabiki.
Mchezo huo dhidi ya Uganda wa marudiano utacheza tarehe 28 Machi siku ya Jumanne saa moja usiku katika Dimba la Benjamin Mkapa. Na kwa kuona umuhimu wa mashabiki katika mchezo huo Cliford Marion Ndimbo alikua pamoja na wasemaji wa Vilabu vya Azam Fc Hashim Ibwe, Simba Ahmed Ally, na Ally Kamwe wa Yanga.
Cliford Ndimbo “Uhitaji wa mashabiki ni mkubwa katika mchezo huo ili kuweza kutoa hamasa kwa wachezaji wetu katika kwenda kufuzu michuano hii ya Afcon kwa mwaka 2023 Ivory Coast.”
Ili kutimiza nafasi ya mchezaji wa 12 katika mchezo huo ambae ni shabiki Marion Ndimbo aliwapigia baadhi ya wadau wa soka ili kuweza kununua tiketi zitakazowawezesha mashabiki wenye uhitaji wakwenda uwanjani wapate tiketi.
“Uhitaji katika mchezo huo ni muhimu sana hivyo tunataka tugawe tiketi kwa mashabiki ili waweze kuingia uwanjani. Hivyo tutaongea na tutawapigia wadau mbalimbali ili waweze kutuchangia tiketi za viwango mbalimbali ili watu wajae kwa wingi,” alisema Cliford Marion Ndimbo.
Viongozi wa serikali, viongozi wa soka pamoja na wadau mbalimbali waliitikia wito huo na kununua tiketi. Baadhi ya wadau waliotoa ahadi za kununua tiketi ni pamoja na Lameck Nyambaya m/kiti DRFA tiketi 200, Hashim Mbaga wa Swahili water tiketi 100, Jesca
Kitambaa cheupe Sinza tiketi 300
Raisi wa Yanga Injinia Hersi Said tiketi 1500,
Mjumbe kamati tendaji Yanga Alex Ngai tiketi 200, Mohamed Soloka Mkurugenzi wa Silent ocean/K4s Security 1000, Mtendaji wa Azam Fc Abdulkarim Popat tiketi 1000, Bulet force security 100, Anthony Mavunde 200.
Pia Waziri Mkuu aliahidi tiketi 2000, tiketi 2000 kutoka Ofisi ya Rais lakini pia kubwa zaidi ni tiketi 100 kutoka kwa muunganilo wa Online Media Fc timu hii ya mpira wa miguu ambayo inahusisha wafanyakazi wa media zote za online nchini.
Mpaka sasa zoezi hilo limefanikiwa kununua tiketi zaidi ya 5000 ambazo zitagawiwa bure kwa mashabiki wapenda soka nchini ili wakaiunge mkono Timu yetu ya Taifa.