Baada ya mchezo kati ya Yanga na Simba kumalizika kwa suluhu ya bila kufungana katika Dimba la Benjamin Mkapa kocha msaidizi wa Yanga amekiri walifanya makosa katika mchezo huo.
Cedrik Kaze ambae ndio alikua kwenye benchi katika mchezo kutokana na kufungiwa kwa Nesradine Nabi alisema walikosea kurudi nyuma katika dakika 20 za mwisho na hivyo kuwapa nafasi Simba kuwashambulia.
“Dakika 20 za mwisho tulifanya makosa ya kurudi nyuma na kumuachia mpinzani kucheza na wakawa hatari langoni kwetu.” Cedrick Kaze
Pia kocha huyo alimzungumzia Mayele kushindwa kufunga katika mchezo huo na kusema haukua mchezo kati yake na Simba.
“Mechi hii haikua ni Mayele dhidi ya Simba, ni mechi kati ya Yanga dhidi ya Simba. Mayele ni mechi ya pili ameshindwa kufunga, alipewa pasi na wenzake na walimsogelea na kussapoti lakini haikua mchezo mzuri kwake.” Alisema Cedrick Kaze.
Kocha Cedrik Kaze pia alikiri ubora wa Simba na ndio sababu ya wao kuweka mipango ya kuwazui wachezaji wao haswa Morrison na Sakho.
“Kila mechi ina aproach yake, Simba ni wazuri kwenye winga zao wana wachezaji wazuri ambao wakiwa mmoja dhidi ya mmoja na ndio maanaa hatukuwaacha kina Sakho na Morrison wakutane na hiyo situation na mabeki wetu” alimalizia Kaze.