Sambaza....

Kocha msaidizi wa klabu ya Yanga Cedric Kaze amesema msimu ujao hatokua na kikosi cha Yanga na tayari anatazamia kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine.

Kaze kocha wa zamani wa Barcelona (U-19) na kikosi cha akiba tayari amehudumu Yanga kwa miaka mitatu na mkataba wake unamalizika June mwaka huu.

“Mkataba wangu unaisha June, na tayari nimeshamwambia Rais wa Klabu sitaongeza tena mkataba,” aliiambia Kickoff Magazine ya nchini Afrika Kusini.

“Nimeshafanya vyakutosha, naamini huu ndio mwisho wazungumo wangu kuwepo hapa. Huwa naamini katika mzunguko. Kazi yangu imeshafanyika hapa, nahitaji kutoka nje na kwenda sehemu nyingine na kujitoa ndani ya hapa.”

Cedrick Kaze.

Kaze akiwa na Yanga amepata medali za kutosha huku kila mwaka katika miaka yake mitatu amekua akipata walau kikombe kimoja ingawa msimu huu ndio umekua mzuri zaidi huku pia akigusia ni wapi ataelekea baada yakuachana na Yanga.

“Nimekaa Yanga miaka mitatu tukiwa hapa tumeshinda Ligi mara mbili, tumeshinda Ngao ya Jamii mara mbili na msimu uliopita tumeshinda ubingwa wa FA na sasa hivi tupo nusu fainali,” alisema na kuongeza 

“Kitu chakwanza naipenda Ligi ya Afrika Kusini na naifwatilia sana, pia ni sehemu ambayo naweza nikafanya kazi pia. Nimekaa Barcelona miaka mitatu, najua mpira pia najua jinsi ya kufanya mawasiliano katika kandanda.” 

Sambaza....