Kocha mkuu wa Yanga ameonekana kumtetea mshambuliaji wake kutoka Ivory Coast na kusema ataendelea kumpa nafasi nyota huyo wa zamani wa Gor Mahia mpaka msimu utakapomalizika.
Luc Aymeal amekiri Yikpe alikua mchezaji mzuri alipokua Gor Mahia lakini haelewi ni kipi kimemkuta nyota huyu mwenye mwili jumba mpaka kushindwa kutamba akiwa na Yanga.
Mashabiki wa Yanga wamekua wakionyesha waziwazi kutokufurahishwa na mshambuliaji huyo aliesajiliwa na Yanga katika dirisha dogo akitokea Kenya katika klabu ya Gor Mahia.
Yikpe mpaka sasa amefunga mabao mawili tu akiwa na Yanga huku mwenyewe akisema hana presha yoyote akiwa na Wanajangwani hao na bado ataendelea kuitumikia klabu hiyo.
Luc Aymael “Sitaki kutoa maoni juu ya [Yikpe], sio mimi ambaye nimesaini mchezaji huyu lakini kwa sasa hatuna uchaguzi mwingi katika eneo la ushambuliaji na lazima nimtumie hadi mwisho wa msimu.
Inaonekana alikuwa mchezaji mzuri wakati alipokua akiichezea Gor Mahia lakini sijui kilichompata, alikuwa tayari nilipokuja, kwa sababu nilimkuta tayari akiichezea Yanga.”