Sambaza....

KOCHA mkuu wa bondia Mfaume Mfaume, Ramadhani Uadi ‘Rama Jah amewauliza mashabiki wa mchezo huo nchini kuwa wanataka mpinzani wa Mfaume kutoka Afrika Kusini apigwe kwenye raundi ya ngapi ili kupunguza maneno ya mashabiki kama iljvyotokea walivyompigia bondia wa Misri kwa KO ya raundi ya pili.

Rama Jah ametoa kauli hiyo kuelekea katika pambano “hata usipolala pata kucha tu” ambalo Mfaume Mfaume ‘Mapafu ya Mbwa’ atapanda ulingoni kuzichapa dhidi ya Nkululeko Mhlongo wa Afrika Kusini kabla ya Seleman Kidunda kumalizana na Eric Mukadi katika pambano ambalo linatarajia kupigwa Juni 30, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar.

Rama Jaha alisema kuwa wamejiandaa vizuri kuelekea katika pambano hilo kwa kumpa heshima ya kutosha mpinzani wao kutokana na rekodi kubwa aliyokuwa nayo lakini bado haijaondoa imani yao ya kuweza kushinda pambano hilo la Juni 30, mwaka huu.

“Binafsi tumejiandaa vizuri na maandalizi yanaendelea kuelekea katika pambano la Juni 30, pale kwenye Ukumbi wa Mlimani City lakini ukweli tunaenda kucheza na mpinzani mgumu ambaye anatekodi na nyota mbili na nusu ambazo bondia wangu hana ila matarajio yetu ni kuweza kupata ushindi kwa sababu nitakuwa na mabondia wawili siku hiyo, Pius Mpenda ambaye ni ndiyo bingwa pekee wa WBU hapa nchini.

Mfaume Mfaume.


“Mpinzani tunamheshimu kwa rekodi yake lakini matarajio yetu ni kumpiga kwa sababu mwarabu ambaye ni bondia namba moja kwao Misri tulimpiga kwa KO ya mapema watu wakasema yule nyanya ila huyu Msauz wanasema mkali sasa watasema wao wanataka tumpige raundi ya ngapi ili kuwesepo maneno tena kama yale yaliojitokeza kwa mwarabu,” alisema Rama Jah.

Pambano hilo ambalo limeandaliwa na Kampuni ya Promosheni ya ngumi za kulipwa nchini PAF Promotion Company Limited ambapo mapambano mengine ya utangulizi yatakuwa kati bondia Fadhili Majiha ‘Stopper’ atakayepanda ulingoni dhidi ya Jamal Kunoga wakati Saleh Kasim atamalizana na Said Bwanga kabla ya Deo Samweli kumvaa Adam Ngange.

Wengine ni Pius Mpenda ambaye atapanda ulingoni dhidi ya Simon Tichecha wa Malawi wakati Rama Jonh Cina akitarajia kupasuana na Yona Segu lakini Omary Maulid atapanda na Shaban Kibiriti na Boniface Seguda atacheza na Hamza Mahamoudu huku Herry Rashid akitarajia kumalizana Hussein Pendeza.

Sambaza....