Sambaza....

Kocha mkuu wa St Louis ya Shelisheli, Ourlie Mathiot, amesema kuwa golikipa wake ndiye alikuwa kikwazo cha Yanga kuweza kupata mabao mengi katika mchezo wa leo uliowakutanisha na mabingwa hao wa Tanzania

Katika mchezo huo wa ligi ya mabingwa Afrika hatua ya awali, ambao Yanga wameibuka wababe kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya klabu hiyo kutoka Shelisheli, bao lililowekwa kambani na mtokea benchi Juma Mahadhi

Golikipa wa St Louis, Mechelle Rama, alifanya kazi kubwa kwa kuokoa hatari nyingi zilizoelekezwa langoni mwake

Aidha Mathiot akimuelezea kipa alisema kuwa alifanikiwa kuwazuia Yanga kupata mabao zaidi

“Kwa hakika amefanya kazi nzuri, na unaweza usigundue lakini aliweza kuipanga vema safu yake ya ulinzi” alisema kocha huyo

Unaweza kusema Yanga walistahili kuibuka na ushindi wa mabao mengi, baada ya kumiliki mpira kwa asilimia kubwa huku wakifanya mashambulizi mengi langoni kwa wapinzani wao hao

Kwa upande wa kocha mkuu wa mabingwa wa Tanzania bara Yanga sc, Mzambia George Lwandamina “GL” amesema bado wananafasi ya kurekebisha makosa yao na kufanya vizuri katika mchezo wa marejeano kule Shelisheli

Sambaza....