Sambaza....

Wekundu wa Msimbazi Simba jana walitupa karata yao yakwanza katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kupata sare ugenini.

Simba walikua katika Dimba la Levy Mwanawasa na kuambulia sare ya mabao mawili kwa mawili mbele ya wenyeji wao Power Dynamos.

 

Baada ya mchezo huo kumalizia kocha wa Simba Robert Oliveira alisema “Tumecheza vizuri hasa kipindi cha pili, tumetengeneza nafasi nyingi,” alisema na kuongeza:

“Tumepoteza nafasi zaidi ya tano za kufunga lakini huu ndio mpira wa miguu tunarudi nyumbani kujipanga.”

Simba iliwalazimu kutoka nyuma mara mbili mbele ya Wazambia hao na kusawazisha ili kujihakikishia sare hiyo muhimi ugenini huku kazi hiyo kubwa ya kusawazisha ilifanya na Clatous Chama akifunga mabao mawili.

Clatous Chama akipiga mpira kufunga bao mbele ya mlinzi wa Power Dynamos.

Katika mchezo huo ilishuhudia mshambuliaji wa Simba Jean Baleke akikosa mabao matatu akiwa peke yake yeye na mlinda mlango wa Power Dynamos.

Katika hatua nyingine mlinzi wa kati Che Fondoh Malone amesema bado timu yao ina nafasi ya kufanya vyema katika mchezo wa marudiano jijini Dar es Salaam.

“Hatujakata tamaa ya kusonga hatua ya makundi, tuna dakika 90 nyingine nyumbani ambazo tunaamini tutazitumia vizuri na kuingia hatua ya makundi,” amesema Che Malone

Sambaza....