Sambaza....

Aliyekua kocha wa Simba Pablo Franco Martin amejiunga na Azamazulu Fc ya nchini Afrika Kusini yenye makazi yake Durban. Pablo aliyeingoza Simba nusu msimu mwaka jana amejiunga na Amazulu kwa miaka mitatu [FAR Post]

Klabu ya Azam Fc itaweka kambi nchini Tunisia ili kujiandaa na msimu ujao wa Ligi, Azam Fc wataondoka nchini July 9 na kikosi kamili tayari kabisa kuweka kambi ya kwaajili ya pre-season. [Mwanaspoti]

Benard Morrison baada ya kuachana na Yanga sasa anatarajiwa kuwa mchezaji wa Singida Fountaine Gate itakayoshiriki michuano ya Afrika katika msimu ujao. [Global Publishers]

Benard Morrison

Cedrick Kaze huenda akasalia Yanga msimu ujao na hii ni inategemea na kocha mpya atakayekuja Yanga, kama atamhitaji basi uongozi utamuongezea mkataba. Kaze pia anahusishwa na Singida Fountaine Gate. [Champion]

Klabu ya Simba inategemea kuweka kambi ya maandalizi nchini Uturuki ili kujiandaa na msimu ujao. Simba itashiriki michuano mipya ya Super Cup msimu ujao [Mwanaspoti]

Rango Chivaviro ataungana na Nasraddine Nabi katika kikosi cha Kaizer Chiefs msimu ujao. Rango aliyehusishwa na Yanga tayari ameshasaini miaka miwili na wababe hao wa Afrika Kusini [Kick off]

Rango Chivaviro 

Nasraddine Nabi anatarajiwa kutangazwa wiki hii na Kazier Chiefs baada ya kukubaliana katika idadi ya watu anaotaka kwenda nao Chiefs, Nabi alitaka wasaidizi wanne lakini Chiefs wamependekeza wawili pekee. [FAR Post].

Bayern Munich wako tayari kumuuza mshambuliaji wa Senegal Sadio Mane, 31, kuondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto, huku Newcastle ikimtaka. [Bild – Ujerumani]

The Red Devils wanafikiria kumnunua kipa wa Inter Milan wa Cameroon, Andre Onana, 27. [Sky Sports Italy]

 

 

Sambaza....