Yanga imemtangaza rasmi Mrithi wa Mwinyi Zahera ambaye alikuwa kocha wa Yanga , Baada ya Mwinyi Zahera kuachana na Yanga , Yanga walibaki na Charles Boniface Mkwasa kama kocha wa muda.
Wamemtaja rasmi Kocha mpya ambaye ni Luc Eymael , ni kocha ambaye ana uzoefu mkubwa sana na soka la Afrika. Kocha huyu ametokea Black Leopards ya Afrika Kusini kuja Tanzania.
Ukifuatalia sehemu ambazo amepita kocha huyo inaonesha asilimia kubwa ya sehemu alizopita amefanikiwa kuchukua kikombe angalau kimoja .
Safari yake ya kwanza kuja Afrika alikuja kwenye klabu ya As Vita , ambapo alifanikiwa kuchukua kombe la Linefoot (2010), na Super Coude De Congo 2011.
Akiwa nchini Gabon na klabu ya Missile alifanikiwa kuchukua Gabon Championat National mwaka 2010.
Akiwa na AFC Leopards ya nchini Kenya alifanikiwa kuwa mshindi wa pili wa Kenyan Premier League 2013, akachukua FKF Presidents Cup 2013.
Rayon Sports ya Rwanda ni sehemu nyingine ambayo aliwahi kuhudumu lakini alichukua nafasi ya pili kwenye ligi kuu ya Rwanda 2013 .
Sehemu nyingine aliyofanikiwa kubeba taji ni Free State Stars ya Afrika Kusini na kuchukua Nedbank Cup 2018