Sambaza....

Kiungo wa Yanga ambaye amemaliza mkataba wake na klabu hiyo ameonekana kuwagonganisha KMC FC na Lipuli FC ambavyo vyote vinataka huduma yake msimu ujao.

KMC FC ambayo imepata nafasi ya kushiriki kombe la shirikisho barani Afrika msimu ujao , inaonekana kutaka kujiimarisha kwa kusajili wachezaji wazoefu.

Ngassa (Yanga, Kushoto) na Kaseja (KMC, Kulia)

Mrisho Ngassa anauzoefu mkubwa kwenye michuano hii ya kimataifa ndiyo maana KMC FC ipo kwenye vita vikali na Lipuli FC ambayo ilikosa nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa baada ya kufungwa na Azam FC kwenye fainali ya kombe la Azam federation Cup.

Kwa upande wa Mrisho Ngassa inaonekana hajatoa uamuzi sahihi wa sehemu anayotaka kwenda kwa sababu yuko kwenye mazungumzo mapya na klabu ya Yanga kuangalia uwezekano wa yeye kuongeza mkataba.

Sambaza....