Baada ya Simba kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila dhdi ya Yanga jana katika mchezo wa raundi ya 26 wa Ligi Kuu ya NBC rekodi zimeandikwa kwa wawili hao haswa kwa upande wa Wananchi Yanga.
Yanga wakiwa valia jezi zao nyeusi ambazo wanaamini ndio jezi zenye bahati kwa upande wao kwa msimu huu walikubali kipigo cha mabao mawili kwa sifuri huku mabao ya Simba yakifunga katika dakika 45 za kwanza na Henock Inonga na Kibu Denis.
Kufuatia kipigo hicho cha mabao mawili kwa sifuri kimewafanya Yanga kutoka uwanjani kwa mara ya kwanza bila kufunga bao katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu. Katika michezo yote ya msimu huu Yanga wamekua wakitoka na bao si tu katika michezo waliyoshinda lakini pia hata mchezo waliopoteza ama kutoka sare.
Katika mchezo dhdi ya Ihefu waliopoteza Yanga walifanikiwa kupata bao moja, lakini pia katika michezo waliyotoka sare dhidi ya Azam ya mabao mawili kwa mawili na mchezo waliotoka sare ya moja kwa moja na Simba bado pia walifanikiwa kupata goli.
Safu ya ushambuliaji ya Yanga inayoongozwa na Fiston Mayele, Kenedy Musonda na Aziz Ki imeonekana kuwa moto katika vilabu vyote vya Ligi Kuu lakini haikufua dafu mbele ya walinzi wa Simba Mohamed Hussein, Shomary Kapombe, Inonga Baka, Joash Onyango na Ally Salim aliyesimama langoni jana kwa mara ya kwanza.
Katika mchezo huo Yanga walifanikiwa kupiga mashuti sita yaliyolenga lango lakini yote yaliishia mikononi mwa mlinda mlango wa Simba Ally Salim huku Fiston Mayele pekee akipiga mashuti matatu yaliyolenga lango.
Kwa upande wa Simba wao wameendeleza ubabe katika Ligi baada ya kufanikiwa kupata ushindi mbele ya Yanga sasa wameendelea kutokufungwa katika Ligi, mara ya mwisho Simba ilipoteza mchezo katika Ligi Kuu ilikua ni Oktoba 27 walipofungwa bao moja bila dhidi ya Azam Fc.
Kwa ushindi huo bado unawaacha Simba wakijichimbia katika nafasi yao ya pili wakipinguza tofauti ya alama na Yanga nasasa zimebaki alama tano.