Sambaza....

Kipa Mwarabu wa Simba ameanza mazoezi na timu pale Morogoro. Ni Ayoub Lakred. Huu ni usajili mzuri. Uzuri wa uzuri hautakuwa kwa Simba peke yake. Itakuwa kwa soka letu kiujumla.

Nitakufafanulia. Kibiashara huyu kipa atakuja kutuletea watazamaji / wafuatiliaji wapya wa mpira wetu kutokea kwao Kaskazini.

 

Ayoub hajatoka timu ndogo. Ametoka timu kubwa. Unadhani ni watu wangapi wataanza kuufuatilia mpira wetu kwa sababu yake? Watakuwa wengi.

Hii ni faida kwa soka letu. Kibiashara hapa tunaweza kupata wawekezaji wengine kutokea Kaskazini.

Ayoub Lakred akiitumikia FAR Rabat.

Kitendo cha Ayoub kuja NBC Premier League watu watataka kujua tuna ligi ya namna gani. Je kama mwekezaji kutokea ukanda huo akiweka fedha zake itamlipa?

Tunavyoona watu wa Afrika Magharibi wanaifuatulia ligi yetu na baadhi ya MAMVP wa ligi zao wanakuja kucheza Tanzania, hii ni hatua na sio bahati mbaya.

Baada ya muda, huenda tukaanza kupokea dili za kibiashara kutokea Magharibi na Kaskazini. Juzi NBC Bank wameweka kiasi kingine kinono cha fedha katika akaunti za mamlaka ya soka letu.

Ayoub Lakred akikaribishwa na wachezaji wenzake wa Simba.

Imeingia Bil 32.5 Hiki ni kiasi kikubwa. NBC Bank hawajatoa pesa hii kama sadaka, kipo walichokiona na kuwavutia. Nadhani tujiandae kupata dili mbalimbali kutoka nje ya Tanzania.

Mpira wetu umeshakuwa mkubwa. Kitendo cha kuona Ayoub anakuja kucheza Afrika Mashariki kipo alichokiona. Tungekuwa bado katika dunia ya kiza ilikuwa ngumu kuwavutia hawa kina NBC, Azam Media kutia fedha zao na hawa kina Ayoub, lakini fedha za wawekezaji zimekuwa chachu kuwavutia wachezaji wa mataifa mbalimbali kuja kucheza ligi yetu.

Hongereni Simba

 

Sambaza....