Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Crescentius Magori amesema uongozi wa timu hiyo umeomba hati nyingine Serikalini baada ya ile ya kwanza kushikiliwa na Mzee Hamisi Kilomoni
Magori amesema mchakato wa kupatiwa hati mpya unaendelea na wakati wowote watakabidhiwa
Magori amesema tayari wamemchukulia hatua Mzee Kilomoni ambapo suala lake limepelekwa Kamati ya Maadili ya TFF
Aidha Magori ametoa ufafanuzi kuwa Mzee Kilomoni sio Mdhamini wa klabu ya Simba kama anavyojitambulisha
“Suala Mzee Hamisi kilomoni tumeamua kumpeleka kwenye kamati ya Maadili ya TFF, kuhusu hati tumeomba hati nyingine Serikalini na tunaipata baada ya ile moja kushikiliwa na kilomoni”
“Hapa karibu tumekuwa na taarifa mbalimbali kuhusu Kilomoni kuwa mdhamini wa klabu yetu ya Simba”
“Amekuwa akipita kwenye vyombo vya habari akieleza habari za klabu yetu.”
“Kuanzia leo tunatangaza kuwa Mzee Kilomoni sio tena mdhamani wa Baraza la Simba na mkataba wake haupo tena, maana mkataba ulimalizika October 2017”
“Na kwa msisitizo zaidi maswala yake tumeyafunga leo hatutaliongelea tena swala lake, zaidi hatua za kisheria zitafuata.”