Sambaza....

MABONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Seleman Kidunda na Mfaume Mfaume ‘Mapafu ya Mbwa’ leo wanatarajia kupima uzito leo Alhamis kabla ya kesho Ijumaa kupanda ulingoni kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar.

Kidunda ambaye atapanda uliongoni dhidi ya Eric Mukadi wa DR Congo wakati Mfaume akitarajia kumvaa Nkululeko Mhlongo wa Afrika Kusini katika pambano lililopewa jina la Hata Usipolala patakucha ambalo limeandaliwa na Kampuni ya PAF Entertainment Company Limited.

Promota wa pambano hilo, Fadhili Maogola alisema kuwa maandalizi ya kuelekea pambano hilo yamekamilika ambapo kesho (leo Alhamisi) watapima uzito kwenye Viwanja vya Leaders Club tayari kwa pambano hilo.

Mfaume Mfaume.

“Maandalizi yanakwenda vizuri kwa sababu mabondia wa nje tayari wameshawasili na tunatarajia Alhamisi ndiyo tutafanya zoezi la kupima uzito kwa mabondia wote kwenye Viwanja vya Leaders Club pale Kinondoni, hii ndiyo itakuwa hata usipolala patakucha na maana yake itaonekana pale Mlimani City kesho Ijumaa.

“Lakini niwakumbushe mashabiki kwamba tiketi zinapatikana kwa bei ambayo naamini kila mdau wa mchezo wa ngumi hatoweza kushindwa kuja kuwapa sapoti mabondia wetu wa hapa ndani kutokana na kubwa wa pambano hili la kimataifa,” alisema Maogola.

Sambaza....