Sambaza....

Mabondia wa ngumi za kulipwa nchini, Seleman Kidunda na Mfaume Mfaume wataongoza mabondia watakaocheza pambano la Hata Usipolala pata kucha kufanya vipimo vya Afya kabla ya pambano hilo linalotarajia kupigwa Juni 30, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar.

Kidunda ametoa kauli hiyo kuelekea katika pambano hilo liliandaliwa na Kampuni ya Promosheni ya ngumi za kulipwa nchini PAF Promotion Company Limited huku pambano hilo likipewa jina la Hata Usipolala pata kucha ambapo pia Mfaume Mfaume ‘Mapafu ya Mbwa’atapanda ulingoni dhidi ya Nkululeko Mhlongo wa Afrika Kusini.

Promota wa pambano hilo kutoka PAF Promotion Company Limited alisema kuwa wanatarajia kufanya vipimo vya afya kabla ya pambano kwa lengo la kufikia kanuni na sheria za mchezo huo kwa mabondia watakaopanda ulingoni kwenye pambano hilo.

Selemani Kidunda.

“Kitu kikubwa ni kwamba kesho (leo) Alhamis mabondia wetu Seleman Kidunda na Mfaume Mfaume watafanyiwa vipimo vya afya kwa mujibu wa sheria ya mchezo wa ngumi ambayo inamtaka bondia kupima afya wiki moja au hata mwezi kabla ya kupanda ulingoni kuweza kupigana.

“Tunafahamu kwamba Kidunda yeye atacheza na Eric Mukadi raia wa DR Congo lakini makazi yake ni Afrika. Kusini ambapo anatokea pia mpinzani wa Mfaume, Nkululeko Mhlongo lakini Pius Mpenda naye atapanda ulingoni kwenye pambano lengine la kimataifa dhidi ya Simon Tcheta wa Malawi,” alisema Maogola.

Mapambano mengine ya utangulizi yatakuwa kati bondia Fadhili Majiha ‘Stopper’ atakayepanda ulingoni dhidi ya Jamal Kunoga wakati Saleh Kasim atamalizana na Said Bwanga kabla ya Deo Samweli kumvaa Adam Ngange.

Wengine ni Pius Mpenda ambaye atapanda ulingoni dhidi ya Simon Tichecha wa Malawi wakati Rama Jonh Cina akitarajia kupasuana na Yona Segu lakini Omary Maulid atapanda na Shaban Kibiriti na Boniface Seguda atacheza na Hamza Mahamoudu huku Herry Rashid akitarajia kumalizana Hussein Pendeza.


Sambaza....